Telegraph: Iran ilipiga na kuharibu kambi 5 za kijeshi za Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i127984-telegraph_iran_ilipiga_na_kuharibu_kambi_5_za_kijeshi_za_israel
Gazeti la Telegraph la Uingereza limefichua kwamba makombora ya Iran yalipiga moja kwa moja vituo vitano vya jeshi vya Israel wakati wa vita vya hivi majuzi vya siku 12, lakini Tel Aviv inaendelea kuficha na kuchuja habari za hasara zilizosababishwa na makombora ya Iran.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jul 05, 2025 23:47 UTC
  • Telegraph: Iran ilipiga na kuharibu kambi 5 za kijeshi za Israel

Gazeti la Telegraph la Uingereza limefichua kwamba makombora ya Iran yalipiga moja kwa moja vituo vitano vya jeshi vya Israel wakati wa vita vya hivi majuzi vya siku 12, lakini Tel Aviv inaendelea kuficha na kuchuja habari za hasara zilizosababishwa na makombora ya Iran.

Telegraph imesema haya kwa mujibu wa data ya rada ambazo haijawekwa wazi kutokana na udhibiti mkali wa jeshi la Israel.

Gazeti la The Telegraph la Uingereza limefichua kuwa, mashambulio ya Iran katika kukabiliana na uvamizi wa siku 12 wa Israel dhidi ya nchi hiyo yalilenga moja kwa moja vituo vitano vya kijeshi vya Israel.

Ripoti ya gazeti hilo imeeleza kuwa makombora ya Iran yalipiga kambi tano tofauti za Israel, lakini mamlaka ya utawala huo haikutangaza mashambulizi hayo ambayo hayakuweza kuripotiwa kutoka ndani kutokana na sheria kali za udhibiti wa kijeshi.

Hata hivyo, wasomi wa Kiamarekani katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Oregon, ambao wamebobea katika kutumia data ya rada za satalaiti kugundua uharibifu wa bomu katika maeneo ya vita, wamelithibitishia gazeti hilo kwamba makombora ya Iran yalipiga moja kwa moja kambi tano za jeshi la Israel, japokuwa Tel Aviv inaendelea kuficha ukweli huo kwa sababu ya udhibiti mkali wa habari zinazohusiana na hasara zilizoipata Israel.

Ripoti zinaonyesha kuwa miongoni mwa vituo vilivyoharibiwa kwa makombora ya Iran ni kambi kubwa ya anga, kituo cha kukusanya taarifa za kijasusi na kambi ya vifaa vya vita, pamoja na mashambulizi 36 yaliyopenya mifumo ya ulinzi wa anga ya Israel, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa miundombinu ya makazi na viwanda.

Inakadiriwa kuwa Marekani ilifyatua kwa uchache makombora 36 ya mfumo wa ulinzi wa anga wa THAAD wakati wa vita vya Israel dhidi ya Iran kwa ajili ya kuzuia makombora ya Jamhuri ya Kiislamu, na kila kombora linagharimu takriban dola milioni 12.