Apr 26, 2024 03:08 UTC
  • Majaliwa: Takriban watu 155 wamefariki dunia nchini Tanzania kutokana na mafuriko

Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alisema jana Alhamisi kuwa takriban watu 155 wamefariki dunia nchini humo kutokana na mvua kubwa inayoambatana na El Nino na hivyo kusababisha mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Tanzania na nchi nyingine za Afrika Mashariki; eneo ambalo linaweza kukabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa  zimekumbwa na mvua kubwa kuliko kawaida katika msimu wa sasa wa mvua huku makumi ya vifo pia vikiripotiwa  katika nchi jirani ya Kenya.

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema kuwa kaya zaidi ya 51,000 na watu 200,000 wameathiriwa na mvua kubwa huku watu 155 wakipoteza maisha na wengine 236 kujeruhiwa. 

Kassim Majaliwa 

Waziri Kassim Majaliwa ameliambia Bunge mjini Dodoma kuwa mvua kubwa za El Nino zilizoambata na upepo mkali, mafuriko na maporomoko ya udongo katika maeneo mbalimbali ya Tanzania yamesababisha maafa na hasara kubwa. Maafa hayo ni pamoja na watu kupoteza maisha, mazao kuharibika, nyumba kujaa maji na kubomoka, na madhara kwa miundombinu kama barabara, madaraja na njia za reli. 

 

Tags