-
'Gaidi', askari 3 na mlinzi wa kampuni binafsi wauawa katika makabiliano ya risasi Tanzania
Aug 25, 2021 12:58Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania (IGP) Simon Sirro meithibitisha habari za kuuawa kwa gaidi,askari watatu na mlinzi wa kampuni binafsi kwenye makabiliano ya risasi yaliyotokea katika eneo la Daraja la Salender jirani na Ubalozi wa Ufaransa, jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo watu sita wamejeruhiwa na imeelezwa kuwa wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Muhimbili.
-
Rais wa Tanzania: Uchaguzi wa 2020 ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana
Aug 21, 2021 14:01Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania ameipongeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kusimamia uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2020 akisema "ulifanyika vizuri sana tena kwa kiwango kikubwa sana."
-
CCM yalisimamisha gazeti lake la ‘Uhuru’ kwa 'kumlisha maneno' rais Samia kuhusu uchaguzi ujao wa rais
Aug 11, 2021 12:43Chama tawala nchini Tanzania, Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema, kitachukua hatua kali dhidi ya watumishi wa gazeti la Uhuru kwa kuandika habari ya upotoshaji juu ya Rais Samia Suluhu Hassan.
-
Raisi: Kuna fursa nzuri za kuimarisha uhusiano wa Iran na Tanzania, Zanzibar
Aug 06, 2021 14:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuna fursa nyingi na nzuri za kuboresha na kustawisha kiwango cha uhusiano baina ya Iran kwa upande mmoja na Tanzania na Zanzibar kwa upande mwingine.
-
Wafuasi wa chama cha upinzani Tanzania Chadema wakamatwa wakiimba "Mbowe sio gaidi"
Aug 05, 2021 12:33Wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho ni chama kikuu cha upinzani Tanzania waliokuwa wamekusanyika nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya korti wamekamatwa na wanashikiliwa na Jeshi la Polisi.
-
Rais Samia Suluhu apewa chanjo ya corona, awatoa hofu Watanzania kuhusu chanjo ya Covid-19
Jul 28, 2021 13:50Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania leo ameongoza zoezi la uzinduzi wa kutoa chanjo ya corona nchini humo akisema asingekuwa tayari kuhatarisha maisha yake kwa kuchanjwa chanjo hiyo kama isingekuwa salama.
-
Corona Tanzania; Marufuku kuingia kwenye usafiri wa umma bila barakoa
Jul 26, 2021 12:28Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam nchini Tanzania, Amos Makalla amewataka Wananchi kuchukuwa tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona ambapo amepiga marufuku wananchi kuingia kwenye vyombo vya usafiri na sehemu za kutoa huduma bila kuvaa barakoa.
-
Wanasheria Tanzania wataka Mbowe ama aachiwe au afikishwe mbele vyombo vya sheria
Jul 25, 2021 11:29Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimeingilia kati sakata la kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kikitaka kiongozi huyo wa upinzani Tanzania ama aachiliwe huru au afikishwe kwenye mamlaka za kisheria.
-
Marais wa Tanzania na Kenya wamtumia salamu za pongezi Rais mteule wa Iran
Jul 24, 2021 08:08Marais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kenya wamemtumia ujumbe Ayatullah Ibrahim Raesi wakimpongeza kwa kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa mwezi uliopita wa Rais hapa nchini.
-
Watu 29 wameaga dunia kwa Corona nchini Tanzania; maambukizo yaongezeka
Jul 24, 2021 04:35Waziri wa Afya wa Tanzania, Dk Dorothy Gwajima amesema hadi sasa jumla ya watu 29 wamefariki dunia kutokana na wimbi la tatu la Covid-19 na kwamba siku ya Alkhamisi pekee kulikuwa na wagonjwa wapya 176.