-
Watanzania washiriki kwa wingi katika upigaji kura leo
Oct 28, 2020 12:27Mamilioni ya Watanzania, leo Jumatano, Oktoba 28, 2020 wamejitokeza katika vituo vya kupigia kura kwa ajili ya kuwachagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, wabunge wa Bunge la Muungano, madiwani na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
-
Watanzania wanapiga kura katika uchaguzi mkuu
Oct 28, 2020 04:47Mamilioni ya raia wa Tanzania leo wanaelekea katika masanduku ya kupiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.
-
Mwito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuelekea uchaguzi mkuu wa Tanzania
Oct 27, 2020 12:54Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), António Guterres ametaka mchakato mzima wa uchaguzi nchini Tanzania kuwa huru na haki.
-
Watu kadhaa waripotiwa kuuawa na kujeruhiwa Pemba, Tanzania katika ghasia za kabla ya upigaji kura ya mapema
Oct 27, 2020 08:20Watu kadhaa wanaoaminika kuwa wafuasi wa chama cha ACT Wazalendo wameripotiwa kuwa wameuawa na kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo kisiwani Pemba, Zanzibar kabla ya kufanyika upigaji kura ya mapema ambao umezusha taharuki visiwani humo.
-
Wasimamizi wa uchaguzi Tanzania watakiwa kufuata sheria
Oct 20, 2020 07:43Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) imewaagiza wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya majimbo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria ili kuepuka malalamiko yanayoweza kusababisha uvunjifu wa amani.
-
Mpwa wa Rais wa Tanzania atishia 'kummaliza' Tundu Lissu kwa sindano ya sumu
Oct 18, 2020 14:13Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM nchini Tanzania ametishia kumuua kwa kumdunga sindano ya sumu, mgombea urais wa nchi hiyo kwa tiketi cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu kwa kile alichosema kuendelea 'kuwajaza upepo' wafuasi wake ili waandamane.
-
Ripoti ya matukio ya Kiislamu juma hili nchini Tanzania + SAUTI
Oct 16, 2020 16:16Viongozi wa dini Tanzania wakemewa na Baraza la Maulamaa la BAKWATA kwa kujihusisha na kuwapigia kampeni wagombea wa vyama vya siasa katika uchaguzi mkuu
-
Kauli ya Mufti wa Tanzania kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28
Oct 16, 2020 07:28Sheikh mkuu na Mufti wa Tanzania Abubakari Zubeir amewataka watanzania kuhakikisha wanailinda amani ya nchi wakati huu ambapo taifa linaelekea kufanya uchaguzi mkuu.
-
Serikali ya Tanzania yatuhumiwa kubana na kukandamiza upinzani kuelekea uchaguzi wa Oktoba 28
Oct 12, 2020 13:56Serikali ya Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania imetunga na kutekeleza sheria kali za kuogofya ili kukandamiza kila aina ya upinzani, wakati nchi hiyo inaelekea kwenye uchaguzi mkuu unaotazamiwa kufanyika tarehe 28 ya mwezi huu wa Oktoba.
-
Polisi visiwani Zanzibar yawaonya vikali wanasiasa 'wachochezi'
Oct 07, 2020 07:57Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar nchini Tanzania amewatahadharisha wanasiasa dhidi ya kutoa matamshi ya kichochezi na uvunjifu wa amani visiwani humo, kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba 28.