-
Asasi za kiraia Tunisia zatilia shaka matokeo ya kura ya maoni
Aug 06, 2022 03:53Asasi za kiraia na mashirika yasiyo ya serikali nchini Tunisia yametilia shaka uhalali wa matokeo ya kura ya maoni ya kubadilisha katiba iliyofanyika zaidi ya wiki moja iliyopita.
-
Al-Ghannouchi: Matokeo ya kura ya maoni ya katiba ya Tunisia ni kichekesho
Jul 28, 2022 11:06Mkuu wa chama chenye mielekeo ya Kiislam cha "Ennahda" nchini Tunisia aliyataja matokeo ya kura ya maoni ya katiba kuwa ni "kichekesho" na kutahadharisha kuhusu uwezekano wa kutokea migawanyiko ndani ya jamii ya Tunisia.
-
Ushiriki mdogo wa Watunisia katika kura ya maoni ya marekebisho ya katiba
Jul 28, 2022 02:23Hatimaye baada ya malumbano mengi, kura ya maoni ya marekebisho ya katiba ya Tunisia ilifanyika siku chche zilizopita licha ya kususiwa na kambi ya upinzani na mashirika mengi ya kiraia.
-
Tunisia yapasisha katiba mpya licha ya wananchi wengi kususia kura ya maoni
Jul 26, 2022 07:07Rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Rais wa Tunisia, Kais Saied imepasishwa licha ya kujitokeza idadi ndogo ya watu katika zoezi la upigaji kura ya maoni lililofanyika jana Jumatatu nchini humo.
-
Kura ya maoni ya katiba mpya yafanyika nchini Tunisia
Jul 25, 2022 07:53Vyombo vya habari vimeripoti kuwa kura ya maoni ya katiba mpya ya Tunisia inafanyika leo nchini humo.
-
Kura ya maoni ya katiba ya Tunisia katika kivuli cha maandamano ya wananchi
Jul 25, 2022 02:28Wakati Tunisia ikiitisha zoezi la kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya, maandamano ya wananchi yanayoendelea nchini humo yamegeuka na kuwa ghasia na machafuko baada ya jeshi kuingilia kati.
-
Watunisia waandamana tena kupinga rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Rais
Jul 24, 2022 07:24Kwa mara nyingine tena, wananchi wa Tunisia wamemimika katika mitaa na barabara za nchi hiyo kushiriki maandamano ya kupinga rasimu ya katiba iliyopendekezwa na Rais wao, Kais Saied.
-
Tunisia:Kiongozi wa chama cha An Nahdhah aachiwa baada ya kusailiwa
Jul 20, 2022 11:52Kiongozi wa chama cha Kiislamu Tunisia cha An Nahdhah ameachiwa huru na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya kuhojiwa kwa muda wa masaa tisa.
-
Taasisi nchini Tunisia zataka kufutwa kura ya maoni kuhusu katiba
Jul 19, 2022 08:07Taasisi 40 na wananchi wa Tunisia wamemtaka Rais wa nchi hiyo Kais Saeid kuacha kuendesha kura ya maoni kuhusu rasimu ya katiba mpya ya nchi hiyo.
-
Ghannouchi: Kais Saied anataka kuimarisha utawala wa kidikteta Tunisia
Jul 16, 2022 07:51Kiongozi wa chama cha Ennahda cha Tunisia, Rached Ghannouchi, amesema kwamba Rais Kais Saied anatumia kura ya maoni juu ya katiba mpya kuimarisha udikteta, akionya kwamba hali ya Sri Lanka inaweza kujikariri nchini Tunisia.