-
Ajali ya basi yasababisha vifo vya watu wasiopungua 20 nchini Uganda
May 04, 2022 14:54Polisi wa Uganda wamesema watu 20 wameuawa baada ya basi la abiria kuanguka kwenye shamba la chai nje ya barabara kuu magharibi mwa Uganda.
-
UNHCR yahitaji dola milioni 47.8 kuwasaidia wakimbizi Uganda
May 01, 2022 04:10Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR na wadau wengine 44 wa misaada ya kibinadamu wametoa ombi la dharura la dola za Marekani milioni 47.8 ili kukabiliana na mahitaji muhimu ya maelfu ya wakimbizi waliofika Uganda mwaka huu, wakikimbia ghasia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na za mapigano ya hapa na pale nchini Sudan Kusini.
-
Viongozi wa Waislamu Uganda wazika tofauti zao, wapania kuunda taasisi moja
Apr 13, 2022 07:58Viongozi wa makundi na mashirika ya Kiislamu nchini Uganda wametangaza kuungana na kusuluhisha tofauti zao, sanjari na kusaini makubaliano ya kuunda taasisi moja itakayowaleta pamoja na kuwaunganisha.
-
EU yaeleza wasiwasi wake kuhusu kambi za mateso nchini Uganda
Apr 07, 2022 11:16Mwakilishi Maalumu wa Umoja wa Ulaya katika Masuala ya Haki za Binadamu ameelezea wasiwasi wake kuhusu kuteswa wafungwa na ukiukwaji mwingine wa haki za binadamu nchini Uganda.
-
Spika wa Bunge la Uganda, Jacob Oulanyah aaga dunia
Mar 20, 2022 12:10Spika wa Bunge la Kitaifa la Uganda, Jacob L'Okori Oulanyah amefariki dunia akitibiwa nchini Marekani.
-
Jeshi la Uganda limekanusha kuwa mtoto wa Museveni amejiuzulu
Mar 14, 2022 13:55Jeshi la Uganda limesema leo Jumatatu kwamba mtoto wa kiume wa Rais Yoweri Museveni, Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye anatajwa kuwa ndiye atakayerithi miikoba ya baba yake kama rais ajaye wa Uganda, hajajiuzulu.
-
ICJ yaiamuru Uganda kuilipa DRC dola milioni 325 tu kufidia gharama za vita
Feb 10, 2022 07:35Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) imetangaza kuwa dola milioni 325 ndio kiasi cha fidia ambacho Uganda inapaswa kuilipa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ilikuwa ikidai zaidi ya dola bilioni 11 kwa uvamizi uliofanywa na jeshi la serikali ya Kampala mashariki mwa nchi hiyo wakati wa vita vya miaka ya 1998-2003.
-
Watanzania 3 wakamatwa DRC wakituhumiwa kuwa wanachama wa ADF
Feb 08, 2022 07:46Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limetangaza habari ya kuwatia mbaroni raia watatu wa Tanzania, kwa tuhuma za kuwa wanachama wa kundi la wanamgambo wa ADF.
-
Viongozi wa Kiislamu Uganda waunga mkono serikali kuhusu mwaka mpya + Sauti
Jan 02, 2022 06:52Serikali ya Uganda imepiga marufuku mijumuiko ya kusherehekea mwaka mpya ili kuzuia maambukizi ya Corona hatua ambayo imeungwa mkono na viongozi wa Kiislamu
-
Rais Museveni asema shule zitafunguliwa Uganda mwezi huu
Jan 01, 2022 12:38Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kuwa, shule za nchi hiyo ambazo zilikuwa zimefungwa tokea Machi 2020 kutokana na msambao wa maradhi ya Covid-19, sasa zitafunguliwa mwezi huu wa Januari, 2022.