-
UN: Mashambulizi ya walowezi wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukingo wa Magharibi yamefikia kiwango cha juu zaidi
Nov 08, 2025 07:57Umoja wa Mataifa umetangaza kwamba walowezi wa Israel wamefanya mashambulizi yasiyopungua 264 dhidi ya Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu mwezi uliopita wa Oktoba, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya kila mwezi tangu maafisa wa Umoja wa Mataifa walipoanza kufuatilia mashambulizi kama hayo mwaka 2006.
-
UN: Israel imekataa maombi zaidi ya 100 ya kuingiza misaada Ghaza tangu vita viliposimamishwa
Nov 07, 2025 10:17Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, tangu yalipoanza kutekelezwa makubaliano ya kusitisha vita tarehe 10 Oktoba, utawala wa kizayuni wa Israel umekataa maombi 107 ya kuingizwa vifaa vya misaada katika Ukanda wa Ghaza, na hivyo kuzuia vifaa muhimu vya kibinadamu kuwafikia Wapalestina wa eneo hilo wanaoishi katika mazingira magumu na ya mateso.
-
UNSC yapitisha azimio la US la kuunga mkono mpango wa Morocco kuhusu Sahara Magharibi
Nov 02, 2025 06:23Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura ya kurefusha kwa mwaka mmoja muda wa kazi za ujumbe wake ulioko Sahara Magharibi (MINURSO), sambamba na kuidhinisha rasmi mpango wa serikali ya Morocco wa kutoa mamlaka ya ndani kwa eneo hilo kama msingi pekee wa kutatua mgogoro huo wa miongo kadhaa, hatua ambayo imesababisha mpasuko mkubwa katika jamii ya kimataifa.
-
Araghchi na Guterres wajadili migogoro ya Gaza, Yemen
Oct 21, 2025 11:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wamefanya mazungumzo ya simu na kuzungumzia matukio ya kikanda ikiwemo hali ya Gaza na Yemen.
-
UN: Makubaliano ya amani ya Kongo na Rwanda 'hayaheshimiwi'
Oct 14, 2025 12:47Umoja wa Mataifa umesema kuwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Rwanda "hayaheshimiwi."
-
Umoja wa Mataifa wakaribisha taarifa ya Hamas kuhusu usitishaji vita Gaza
Oct 04, 2025 07:31Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekaribisha kwa mikono miwili taarifa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas inayoonyesha utayarifu wake wa kuwaachilia mateka na kukubali kwa masharti mpango wa Rais wa Marekani Donald Trump wa kusitisha mapigano katika Ukanda wa Gaza.
-
Je, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limenasa katika mtego wa kura ya turufu?
Oct 01, 2025 02:32Haki ya kura ya turufu ni mojawapo ya masuala yenye utata kuhusu mamlaka ya wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Iran yalaani urejeshaji vikwazo vya UN vilivyokwisha muda wake uliofanywa na Marekani na Ulaya
Sep 30, 2025 07:34Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi ameikosoa Marekani na mataifa matatu ya Ulaya kwa kujaribu kutumia utaratibu wa 'snapback' wa makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 ili kurejesha tena vikwazo vilivyokwisha muda wake vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.
-
Iran: Wanachama wa UN hawana wajibu wa kuheshimu maazimio batili dhidi ya Tehran
Sep 29, 2025 02:26Iran imesema madai yaliyotolewa na Marekani na nchi za Ulaya kuhalalisha kurejeshwa kwa maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya nchi hii hayaziwajibishi nchi wanachama wa UN kuzingatia na kuheshimu hati za umoja huo zilizobatilishwa hapo awali.
-
Vipi Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limefikia natija ya kufanyika mauaji ya kimbari huko Gaza?
Sep 29, 2025 02:16Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limetangaza hatua za Israel huko Gaza kuwa ni mfano wa kisheria wa "mauaji ya halaiki."