-
UN yatahadharisha: Al-Shabab bado ni tishio kubwa nchini Somalia na Kenya
Dec 26, 2025 08:24Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wametahadrharishakatika ripoti yao wiki hii kwamba kundi lenye misimamo mikali la al Shabab lingali ni tishio kubwa hivi sasa kwa amani na uthabiti huko Somalia na katika eneo zima pa Pembe ya Afrika ikiwa ni pamoja na katika nchi jirani ya Kenya.
-
UN yalaani vikali shambulio la kigaidi lililoua waumini msikitini jimboni Borno, Nigeria
Dec 25, 2025 23:53Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio la kigaidi lililotokea kwenye msikiti ulioko katika Soko la Gamboru, mjini Maiduguri, katika Jimbo la Borno kaskazini-mashariki mwa Nigeria, lililopelekea kuuawa na kujeruhiwa makumi ya Waislamu waliokuwemo msikitini humo.
-
Mwakilishi wa Iran UN: Baada ya Oktoba 2025, Azimio 2231 halikuwa tena na itibari ya kisheria
Dec 24, 2025 03:17Mwakilishi wa Iran katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa cha kujadili Azimio 2231 amesema, Jamhuri ya Kiislamu inakubaliana na misimamo ya Russia na China ya kupinga kuitishwa kwa kikao hicho. Azimio 2231 lina kifungu kinachoeleza bayana kwamba muda wake wa kumalizika ni Oktoba 2025, na baada ya hapo hakutakuwa tena na msingi wa kisheria wa kuendelea majukumu ya azimio hilo.
-
Kuzidi kuwa tata vita vya Sudan; indhari ya Umoja wa Mataifa kuhusu kupanuka wigo wake
Dec 23, 2025 08:24Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa sanjari na kusisitiza umuhimu wa kusitisha vita nchini Sudan, ameonya kuhusu utambulisho wake tata na athari zake zinazopanuka kwa nchi jirani na eneo kwa ujumla.
-
UN: Usafirishaji bidhaa duniani kote karibuni hivi utakuwa wa kasi na wa gharama nafuu zaidi
Dec 18, 2025 23:55Usafirishaji wa bidhaa kote duniani unatazamiwa kuwa wa gharama nafuu zaidi, unaofanyika kwa kasi zaidi na kwa urahisi mkubwa, kufuatia kupitishwa makubaliano mapya yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambayo yanahuisha nyaraka zinazotumika katika usafirishaji wa kimataifa.
-
UN yalaani shambulio lililoua askari 6 wa kulinda amani Sudan
Dec 13, 2025 23:06Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ameeleza kusikitishwa na shambulio la ndege isiyo na rubani lililolenga kituo cha Umoja wa Mataifa nchini Sudan, na kuwaua askari sita wa kulinda amani wa umoja huo.
-
UN: Kuna hatari ya kuzuka wimbi jipya la mashambulizi na janga la kibinadamu Kordofan, Sudan
Dec 04, 2025 23:27Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametoa indhari kuhusu hatari ya kuzuka wimbi jipya la ukatili katika eneo la Kordofan, Sudan, baada ya kushadidi mapigano kati ya Jeshi la Sudan (SAF), Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) na Kundi la Harakati ya Kaskazini ya Ukombozi wa Wananchi wa Sudan, (SPLM-N).
-
Azimio la UN: Israel inaikalia "kinyume cha sheria" Miinuko ya Golan ya Syria, iondoke kikamilifu
Dec 03, 2025 07:24Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio linalotangaza kuwa, kuendelea Israel kuikalia kwa mabavu na kuiunganisha na upande wake Miinuko ya Golan ya Syria ni "kinyume cha sheria" na limeutaka utawala huo uondoke kikamilifu katika eneo hilo hadi kwenye mstari wa mpaka wa Juni 4, 1967.
-
Guterres: UN inafuatilia hali ya Guinea-Bissau 'kwa wasiwasi mkubwa' baada ya jeshi kufanya mapinduzi
Nov 26, 2025 23:27Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa anafuatilia matukio ya Guinea Bissau kwa wasiwasi mkubwa baada ya baada ya jeshi la nchi hiyo jana Jumatano kumuondoa madarakani Rais Umaro Sissoco Embalo wa nchi hiyo.
-
WHO: Ukatili dhidi ya wanawake ungali ni janga kubwa la haki za binadamu
Nov 20, 2025 02:38Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) pamoja na wadau wa Umoja wa Mataifa wametoa ripoti muhimu inayoonyesha kuwa ukatili dhidi ya wanawake ungali ni janga kubwa la haki za binadamu, kwa sababu takwimu za zaidi ya miaka 20 zinaonesha kutokuwepo kwa hatua kubwa zilizopigwa katika kupunguza ukatili huo.