-
Wananchi wa Morocco wateketeza moto bendera za Israel katika maandamano
Aug 09, 2022 06:29Wananchi wa Morocco waliokuwa na hasira wameteketeza moto bendera za utawala wa Kizayuni wa Israel mbele ya bunge la nchi hiyo katika maandamano ya kulaani hujuma ya utawala huo dhidi ya Gaza.
-
HAMAS: Kuanzisha uhusiano na Wazayuni ndio sababu ya kushadidi jinai dhidi ya Wapalestina
Aug 06, 2022 22:29Msemaji wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS amesema, mwenendo wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ndio unaohamasisha utawala huo dhalimu kushadidisha jinai zake dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Iran yalaani hujuma ya Gaza iliyotekelezwa na utawala wa apathaidi wa Israel
Aug 06, 2022 02:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani hujuma ya kuogofya ya utawala wa apathaidi wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza na kusema: "Palestina ina haki ya kisheria ya kujilinda mbele ya hatua za kigaidi za Israel"
-
Wazayuni: Jihad al Islami imeweka tayari zaidi ya makombora 3000 yakisubiri kufyatuliwa tu
Aug 05, 2022 23:22Duru za Kizayuni zimedai kuwa, Harakati ya Jihad al Islami ya Palestina imeweka tayari kwa ajili ya kufyatuliwa makombora zaidi 3000 baada ya kiongozi wake mmoja kukamatwa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Tawi la kijeshi la HAMAS lawaonyesha askari wawili wa Israel linaowashikilia mateka
Jul 31, 2022 07:10Brigedi za Izzuddinul-Qassam, tawi la kijeshi la Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina, HAMAS zimetoa taswira, sambamba na kuwahutubu Wazayuni kwamba: viongozi wa utawala wa Kizayuni wanakuambieni uongo kuhusu mateka.
-
Sheikh Naim Qassem: Israel haina budi kutambua rasmi haki za maliasili za Lebanon
Jul 31, 2022 07:04Naibu Katibu MKuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema, utawala haramu wa Kizayuni wa Israel hauna budi kuzitambua rasmi haki za Lebanon zinazohusiana na utajiri wa maliasili za baharini.
-
Iran: Mpango wa kijeshi wa nyuklia wa Israel ni tishio kwa usalama wa dunia
Jul 29, 2022 23:51Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema ustawi wa mpango wa kijeshi wa nyuklia wa utawala wa Kizayuni wa Israel na kuendelea kukataa utawala huo vituo vyake vya nyuklia vikaguliwe na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ni tishio kubwa kwa usalama wa kimataifa.
-
Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran: Kamera za usalama kwa sasa hazitawashwa
Jul 25, 2022 06:50Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa, iwapo tuhuma dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran zitaendelezwa hakuna sababu ya kuwepo kamera katika taasisi za nyuklia za Iran.
-
Baada ya kutimuliwa Russia, shirika la uhajiri wa Mayahudi kuhamishiwa Israel
Jul 25, 2022 03:44Sambamba na kushadidi mivutano katika uhusiano wa Russia na Israel, duru za habari zimeripoti kuwa shirika la uhajiri wa Mayahudi limeandaa mpango wa siri wa kuhamishia Palestina inayokaliwa kwa mabavu (Israel) ofisi yake iliyokuweko mjini Moscow.
-
Maulamaa wa Beirut: Lebanon katu haitaanzisha uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni
Jul 25, 2022 03:25Baraza la Maulamaa wa Beirut limesisitiza kuwa hakuna mahusiano yoyote ya kibinadamu au ya kidini baina ya Lebanon na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel kwa sababu kulingana na katiba utawala huo ni adui wa Lebanon.