Jul 25, 2022 11:20 UTC
  • Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran: Kamera za usalama kwa sasa hazitawashwa

Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amesema kuwa, iwapo tuhuma dhidi ya miradi ya nyuklia ya Iran zitaendelezwa hakuna sababu ya kuwepo kamera katika taasisi za nyuklia za Iran.

Baada ya kusimama mazungumzo ya Vienna ya kuindolea Iran vikwazo, na Marekani kushindwa kurejea katika mapatano ya JCPOA kutokana na Washington kutokuwa na azma thabiti ya kisiasa; nchi hiyo na Troika ya Ulaya inayoundwa na nchi tatu za Ujerumani, Uingereza na Ufaransa zilipasisha azimio dhidi ya Iran kufuatia mashinikizo ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Rafael Grossi Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA). 

Mapatano ya nyuklia ya JCPOA 

Azimio hilo limepuuza ushirikiano mkubwa wa Iran na wakala wa IAEA ambao umekuwa ukiendelea kwa nia njema; na ndio maana Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran pia limetangaza kusitishwa shughuli za ufungaji kamera za usalama katika kituo cha wakala huo.  

Kkuhusu ushirikiano wa Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) Muhammad Eslami, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran leo Jumatatu amesema mbele ya mkutano na waandishi wa habari kwamba, mapatano wa JCPOA ni natija ya mazungumzo kati ya Iran na kundi la 5+1, hata hivyo nchi za Magharibi zinaendelea kuituhumu Iran kwa kutumia nyaraka zilizoibwa na kutoa madai mbalimbali.

Eslami ameongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikubali mapatano ya JCPOA kwa msingi wa kufutwa tuhuma dhidi yake na kujenga hali ya kuaminiana.  Aidha Iran ilikubali kupunguza shughuli za miradi yake ya nyuklia ili kujenga imani, hata hivyo upande wa pili umeshindwa kutekeleza majukumu na ahadi zake katika uwanja huo.

Tags