-
Hamaki ya Tel Aviv dhidi ya matamshi ya Papa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni
Dec 26, 2024 13:38Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya utawala wa Kizayuni wa Israel imemwita balozi wa Vatican katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu kwa ajili ya kusailiwa. Ni baada ya Papa Francis, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani kukosoa vita na mauaji ya Israel katika Ukanda wa Gaza.
-
Barua ya Iran kwa Baraza la Usalama baada ya Israel kukiri ilihusika na mauaji ya Ismail Haniyeh
Dec 25, 2024 12:07Amir Saeid Iravani, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Umoja wa Mataifa jana Jumanne alimwandikia barua Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Mkuu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisisitiza kwamba, Israel imebeba dhima ya kuhusika na mauaji ya Shahidi Ismail Haniyeh, mkuu zamani wa Idara ya Siasa ya harakati ya Hamas.
-
Maulamaa wa Yemen wautaka Umma wa Kiislamu kukabiliana na mashambulizi ya Wazayuni na Marekani
Dec 25, 2024 03:48Maulamaa wa Yemen wameutaka Umma wa Kiislamu kukabiliana na mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Isreal na Marekani huko Gaza, Yemen na pia waungaji mkono wa kigaidi.
-
HAMAS: Wapalestina wapambane kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Palestina
Dec 24, 2024 11:49Afisa mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS ametoa wito wa kufanyika "hamasa kubwa ya umma" kwa lengo la kuondoa mzingiro wa kinyama uliowekwa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina (PA) kwenye kambi ya wakimbizi ya Jenin, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu.
-
Wazayuni wayafanya maisha kuwa magumu huko Jabalia, Ukanda wa Gaza
Dec 23, 2024 14:01Wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wameifanya hali ya mambo na maisha kuwa ngumu katika eneo la Jabalia kwa lengo la kuwahamisha kwa nguvu wakazi wa Kipalestina wa mji huo.
-
Mjumbe wa Ansarullah: Utawala wa Kizayuni hauna ubavu wa kukabiliana na vikosi vyetu peke yake
Dec 23, 2024 05:50Mjumbe Mwandamizi wa ofisi ya kisiasa ya Harakati ya Ansarullah ya Yemen amesisitiza kwa kusema: "mashambulizi yetu yaliukanganya mfumo wa ulinzi wa anga wa Marekani na kupelekea kutunguliwa ndege ya kivita ya Marekani kwa shambulio lao wenyewe" na akaongeza kuwa utawala wa Kizayuni hauna ubavu wa kukabiliana na Wayemen peke yake na ndio maana unaomba msaada kwa watu wanaouunga mkono.
-
Balozi wa Yemen Tehran: Wayemen wamevuruga uchumi wa utawala wa Kizayuni kwa mashambulizi yao
Dec 22, 2024 08:10Balozi wa Yemen mjini Tehran, Iran, amesema kuwa wananchi wa Yemen wamefanikiwa kuvuruga uchumi wa utawala wa Kizayuni kwa kutekeleza oparesheni zao za kijeshi katika Bahari Nyekundu dhidi ya utawala huo; na hasa uchumi wa bandari ya Ailat ambayo ni bandari kubwa zaidi ya utawala wa Kizayuni ambayo imetangaza kufilisika.
-
Al Houthi: Mifumo ya ulinzi wa anga haiudhaminii usalama utawala wa Kizayuni
Dec 22, 2024 03:41Muhammad Ali al Houthi mjumbe wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amezungumzia mashambulizi ya makombora ya nchi hiyo dhidi ya Israel na kusisitiza kuwa mifumo ya ulinzi wa anga ya utawala wa Kizayuni haiudhaminii usalama utawala huo.
-
Kombora la Yemen lapiga katikati ya Tel Aviv na kujeruhi watu 14, Israel yakiri imeshindwa kulitungua
Dec 21, 2024 03:42Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limetangaza kuwa kombora lililorushwa kutoka Yemen usiku wa kuamkia leo limepiga katikati ya mji mkuu wa utawala huo haramu Tel Aviv baada ya mifumo yake ya ulinzi wa anga kushindwa kulinasa na kulitungua.
-
Umoja wa Mataifa: Mashambulizi ya anga ya Israel nchini Syria lazima yasitishwe
Dec 20, 2024 07:59Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, mashambulizi ya anga ya utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Syria ni ukiukaji wa mamlaka ya kujitawala na utimilifu wa ardhi ya nchi hiyo.