-
Familia za mateka Waisrael zaanzisha mgomo wa nchi nzima kupinga upanuzi wa vita dhidi ya Ghaza
Aug 17, 2025 23:24Gazeti la Times of Israel limeripoti kuwa familia na waungaji mkono wa mateka Waisrael wameanza mgomo wao wa nchi nzima ili "kupinga upanuzi wa vita katika Ukanda wa Ghaza badala ya kusaini makubaliano ya kufanikisha kuachiliwa huru mateka hao wanaoshikiliwa na Hamas".
-
Jumapili, 17 Agosti 2025
Aug 16, 2025 22:58Leo ni Jumapili 23 Mfunguo Tano Safar 1447 Hijria mwafaka na Agostu 17 2025 Miladia.
-
UN: Israel imeshaua Wapalestina wasiopungua 1,760 Ghaza wanaokimbilia msaada wa chakula
Aug 16, 2025 03:09Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa tangu mwishoni mwa mwezi Mei hadi sasa, jeshi la Israel limeshawaua Wapalestina wasiopungua 1,760 walipokuwa wakihangaika kupata msaada wa chakula huko Ukanda wa Ghaza likiwa ni ongezeko la mamia kadhaa tangu ilipotoa takwimu zake za mwisho mwanzoni mwa mwezi huu wa Agosti.
-
Je, nchi za Amerika ya Kusini zimepokea vipi mpango wa Israel wa kukalia kwa mabavu Gaza?
Aug 15, 2025 22:47Nchi nyingi za Amerika ya Kusini zimekuwa na misimamo ya kukosoa waziwazi mpango wa utawala wa Kizayuni wa kuikalia kijeshi Gaza. Bila shaka, baadhi ya nchi, kama vile Argentina, zimechukua msimamo tofauti wa kuiunga mkono Tel Aviv.
-
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran: Muqawama ni 'hazina kubwa' kwa eneo
Aug 15, 2025 04:01Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amesema, Muqawama ni "hazina kubwa" kwa eneo na Ulimwengu wa Kiislamu na akabainisha kuwa makundi ya Muqawama yamefikia kwenye "ukomavu" katika kujichukulia maamuzi yao.
-
HAMAS: Mpango wa Netanyahu wa 'Israel Kubwa Zaidi' ni tishio la wazi kwa mataifa ya Kiarabu na Waislamu
Aug 15, 2025 04:00Kiongozi mwandamizi wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu wa Palestina HAMAS ametahadharisha kuhusu kupanuliwa kwa mipango ya ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa kizayuni katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na kueleza kwamba hatua hiyo inakwenda sambamba na matamshi na ndoto za Benjamin Netanyahu kuhusu kuasisi "Israel Kubwa Zaidi."
-
Wabunge wa UK wamwandikia barua waziri mkuu kumtaka 'amtimue haraka sana' balozi wa Israel
Aug 15, 2025 03:48Wabunge kadhaa wa Uingereza wametoa wito wa kufukuzwa haraka sana balozi wa utawala wa kizayuni wa Israel nchini humo Tzipi Hotovely na kuchukuliwa hatua za haraka za kukabiliana na mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Ghaza pamoja na kuuwekea vikwazo vya silaha utawala huo haramu.
-
Takwimu za kutisha za watoto wahanga wa njaa na vita Gaza
Aug 14, 2025 03:13Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) amesema kuhusu ukubwa wa maafa ya kibinadamu huko Gaza kwamba, mamia ya watoto wamekufa kutokana na njaa na utapiamlo, na makumi ya maelfu ya wengine wamekuwa wahanga wa mashambulizi ya anga ya Israel.
-
Shambulio la ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni kusini mwa Lebanon
Aug 13, 2025 03:46Duru za Lebanon zimeripoti kuhusu shambulio la ndege zisizo na rubani za utawala wa Kizayuni kwenye bandari ya "Al-Naqourah" iliyoko kusini mwa Lebanon.
-
Rais wa Uturuki: Baada ya miaka 80 lazima UN ifanyiwe mageuzi makubwa ili kutimiza wajibu wake
Aug 12, 2025 03:28Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema, wakati Umoja wa Mataifa unakaribia kuadhimisha miaka 80 ya kuasisiwa kwake ni wazi kwamba unahitaji mabadiliko makubwa ili kuendelea kutekeleza majukumu uliyopewa.