-
Kuongezeka kukosolewa uungaji mkono wa Magharibi kwa utawala wa Kizayuni
Nov 16, 2023 00:41Kuendelea jinai , mauaji ya kimbari na kutokomezwa kizazi cha wananchi wa Gaza na utawala wa Kizayuni ambazo zimesababisha maelfu ya Wapalestina kuuawa shahidi na kujeruhiwa, kumepelekea kushtadi kukosolewa siasa za upendeleo za serikali za Magharibi kwa Israel.
-
Uungaji mkono wa Magharibi kwa utawala wa Kizayuni: Sababu ya chuki dhidi ya uyahudi ulimwenguni
Nov 15, 2023 00:24Kushadidi jinai za Israel dhidi ya Wapalestina na uungaji mkono wa pande zote wa nchi za Magharibi kwa mauaji ya kimbari ya utawala wa Kizayuni kumepelekea kuongezeka chuki dhidi ya Uyahudi duniani, kiasi kwamba Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa katika barua yake amelaani ongezeko hilo la chuki dhidi ya uyahudi katika nchi hiyo na kuonya juu ya ukuaji usiovumilika wa chuki dhidi ya Wayahudi.
-
Upinzani wa Wamagharibi kwa usitishaji vita Gaza
Nov 14, 2023 05:53Licha ya kupita karibu siku 40 tangu ilipotokea operesheni ya kimbunga ya Al-Aqswa na radiamali ya utawala wa Kizayuni kwa operesheni hiyo kwa kushambulia kwa mabomu Ukanda wa Gaza na kuuawa maelfu ya Wapalestina na uharibifu mkubwa wa eneo hilo, lakini baadhi ya madola ya Magharibi yakifungamana na Waziri Mkuu wa utawala huu, Benjamin Netanyahu, bado yangali yanapinga usitishaji wa vita hivi vya umwagaji damu.
-
Kuadhibiwa waungaji mkono wa Palestina katika vyuo vikuu vya Marekani
Nov 12, 2023 23:17Licha ya madai ya kuheshimiwa uhuru wa kujieleza katika nchi za Magharibi ikiwemo Marekani, lakini ukweli wa mambo ni kwamba kuna mistari miekundu katika uwanja huo, likiwemo suala la kutetea kadhia ya Palestina, ambapo waungaji mkono wa taifa hilo linalodhulumiwa hukabiliwa na vikwazo vya aina mbalimbali vikiwemo vya kuadhibiwa na kufungwa jela.
-
Rais Raisi: Utawala wa Kizayuni ndio chimbuko la masaibu mengi ya dunia yakiwemo ya Afrika
Nov 11, 2023 23:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekutana na kuzungumza na Mkuu wa Baraza la Utawala wa Sudan na kuutaja utawala wa Kizayuni kuwa balaa kubwa kwa Umma wa Kiislamu na ulimwengu mzima.
-
Kuongezeka hasira za kimataifa kuhusu jinai za utawala wa Kizayuni huko Gaza
Nov 11, 2023 23:37Sambamba na kuendelea vitendo vya jinai vya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, ambavyo hadi sasa vimepelekea kuuawa shahidi zaidi ya Wapalestina elfu 11 na kujeruhiwa wengine zaidi ya elfu 27, hasira na ukosoaji wa kimataifa unaendelea kuongezeka kwa kadiri kwamba mbali na maandamano makubwa yanayofanyika katika pambe tofauti za dunia, baadhi ya wanasiasa wa Magharib pia wanaukosoa utawala huo kutokana na ukatili wake wa kutisha dhidi ya Wapalestina wasio na hatia.
-
Nukta tano muhimu katika barua ya Islami kwa Grossi kuhusiana na tishio la utawala wa Kizayuni kutumia bomu la nyuklia dhidi ya Ghaza
Nov 11, 2023 07:32Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amelitaka shirika hilo kulibainishia wazi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hatari zinazoweza kusababishwa na matumizi au tishio la matumizi ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Idadi ya wanajeshi wa Kizayuni walioangamizwa yafika 365
Nov 11, 2023 03:30Idadi ya askari na maafisa wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel waliouawa tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefika 365.
-
Netanyahu akataa ombi la Biden la kusitisha mapigano kwa siku 3 huko Gaza
Nov 08, 2023 22:48Rais Joe Biden wa Marekani amemtaka Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel asitishe mapigano kwa siku tatu ili kutatua suala la mateka. Kuhusiana na jambo hilo, Biden amesema katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika siku ya Jumanne alimuomba Benjamin Netanyahu asitishe mapigano ili kuandaa uwanja wa kushughulikiwa suala la mateka wa Israel.
-
Siku ya 33 ya vita Gaza; waliouawa shahidi kwa mashambulio ya kinyama ya Israel wafikia 10,569
Nov 08, 2023 08:55Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa idadi ya waliouawa shahidi kutokana na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni katika eneo hilo imeongezeka na kufikia 10,569.