Idadi ya wanajeshi wa Kizayuni walioangamizwa yafika 365
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i104628-idadi_ya_wanajeshi_wa_kizayuni_walioangamizwa_yafika_365
Idadi ya askari na maafisa wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel waliouawa tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefika 365.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Nov 11, 2023 03:30 UTC
  • Idadi ya wanajeshi wa Kizayuni walioangamizwa yafika 365

Idadi ya askari na maafisa wa jeshi la utawala ghasibu wa Israel waliouawa tangu tarehe 7 Oktoba hadi sasa imefika 365.

Hayo yameelezwa na Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala haramu wa Kizayuni wa Israel ambaye ameongeza kuwa, idadi ya wanajeshi na maafisa wa utawala huo wanaouawa inazidi kuongezeka.

Wakati huo huo, jana jeshi la utawala ghasibu wa Israel lilithibitisha kuuawa askari wake mwingine huko Gaza na kuifanya idadi ya askari wake waliouawa tangu kuanza kwa operesheni ya ardhini ya jeshi hilo kufikia 36.

Katika upande mwingine, Radio ya Israel imetangaza kuwa, wanajeshi watano wa Israel wamejeruhiwa kufuatia mashambulio ya ndege zisizo na rubani na mashambulio ya makombora  yaliyorushwa kutoka Lebanon na kulenga maeneo ya kaskazini mwa Israel (Palestina inayokaliwa kwa mabavu).

Katika jibu ililotoa kwa madhila ya zaidi ya miongo saba ya kukaliwa kwa mabavu Palestina na zaidi ya miaka kumi na tano ya kuwekewa mzingiro Gaza na kufungwa jela na kuteswa maelfu ya Wapalestina, mnamo tarehe 7 Oktoba, Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) ilianzisha operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa.

 

Operesheni hiyo inachukuliwa kuwa moja ya mashambulio makali zaidi dhidi ya utawala dhalimu wa Kizayuni.

Wapiganaji wa Hamas walipenya kwenye maeneo yanayokaliwa kwa mabavu kupitia nukta kadhaa za uzio wa mpakani na kushambulia vijiji kadhaa, ambapo mbali na kuangamiza idadi kubwa ya Wazayuni, waliwakamata mateka wengine kadhaa miongoni mwao.