-
Wazayuni waliojifanya kusaidia wahanga wa matetemeko Uturuki kumbe ni wezi!
Feb 20, 2023 22:59Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya Palestina amefichua kuwa, timu ya utawala wa Kizayuni iliyojipeleka Uturuki kwa madai ya kusaidia wahanga wa mitetemeko ya ardhi, wameiba nyaraka za kihistoria ya Uturuki.
-
Imamu wa Swala ya Ijumaa Tehran akosoa mienendo ya Wamagharibi kuhusu tetemeko la ardhi nchini Syria
Feb 17, 2023 10:02Imam wa Swala ya Ijumaa ya leo mjini Tehran amekosoa mienendo ya nchi za Magharibi kuhusiana na tetemeko la ardhi nchini Syria.
-
Walionusurika 'kimiujiza' kwenye zilzala ya Uturuki waendelea kupatikana, vifo vyakaribia 44,000
Feb 17, 2023 04:23Taarifa za uokokaji wa 'kimiujiza' zinaendelea kutolewa kutoka maeneo yaliyokumbwa na tetemeko la ardhi la Februari 6 katika nchi za Uturuki na Syria, huku watu wengine wanne wakitolewa wakiwa hai kwenye majengo yaliyoporomoka nchini Uturuki zikiwa zimepita zaidi ya siku 10 tokea lilipotokea tetemeko hilo.
-
UN yawasilisha ombi la msaada wa dola bilioni moja kusaidia waathirika wa Zilzala Uturuki
Feb 17, 2023 04:02Umoja wa Mataifa umezindua ombi la dola bilioni moja kwa ajili ya usaizidi wa kibinadamu kwa wananchi wa Uturuki wanaokumbwa na machungu kufuatia tetemeko kubwa zaidi la ardhi kuwahi kukumba taifa hilo katika kipindi cha karne.
-
Wananchi wa Uturuki waliokumbwa na mitetemeko walishukuru Jeshi la Iran kwa msaada wa tiba
Feb 15, 2023 09:00Wananchi wa eneo lililokumbwa na mitetemeko mikubwa ya ardhi la Adıyaman nchini Uturuki wamelishukuru Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu kwa kujenga hospitali ya muda inayowahudumia waathirika katika eneo hilo.
-
Baada ya kupita siku 5, manusura wa tetemeko la ardhi waendelea kupatikana vifusini nchini Uturuki
Feb 11, 2023 08:27Watu kadhaa wameokolewa leo nchini Uturuki kwa kutolewa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka, wakati vikosi vya uokoaji kutoka nchi mbalimbali duniani vikiongeza kasi ili kujaribu kuokoa maisha ya watu zaidi baada ya matetemeko makubwa ya ardhi yaliyotokea siku ya Jumatatu kusini mwa nchi hiyo na katika nchi jirani ya Syria.
-
Idadi ya waliofariki dunia yapindukia 24,000 zilzala ya Syria na Uturuki, matumaini ya kupata manusura zaidi yanafifia
Feb 11, 2023 03:56Matumaini ya kupata manusura zaidi chini ya vifusi vya nyumba zilizobomolewa na zizlala ya Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki yanazidi kupungua siku 5 baada ya maafa ya tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 24,000 na kujeruhi makumi ya maelfu ya wengine.
-
Umoja wa Mataifa wakiri kuingizwa masuala ya kisiasa katika kadhia ya kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi nchini Syria
Feb 10, 2023 22:48Rola Amin, Msemaji wa Kamishna Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi, UNHCR amesema misimamo ya kisiasa inapaswa kuwekwa kando na juhudi kufanyika kwa ajili ya kuwafikishia misaada ya kibinadamu waathirika wa tetemeko la ardhi nchini Syria.
-
Mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
Feb 10, 2023 03:52Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wamejadili kuhusu matukio ya kieneo na kimataifa, ikiwa ni pamoja na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea karibuni nchini Syria na Uturuki, na hali ya mazungumzo ya kuiondolea Iran vikwazo vya kidhulma.
-
Venezuela yaonyesha mshikamano wake kwa Uturuki na Syria; yatuma misaada ya kibinadamu kwa waathirika wa zilzala
Feb 08, 2023 22:49Kikosi cha waokoaji 52 wa Venezuela na wahudumu wa idara ya zima moto waliondoka jana Jumatano Caracas wakielekea katika nchi za Uturuki na Syria kwa ajili ya operesheni ya uokoaji wa waathirika wa tetemeko la ardhi lililozikumba nchi hizo.