Wazayuni waliojifanya kusaidia wahanga wa matetemeko Uturuki kumbe ni wezi!
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya Palestina amefichua kuwa, timu ya utawala wa Kizayuni iliyojipeleka Uturuki kwa madai ya kusaidia wahanga wa mitetemeko ya ardhi, wameiba nyaraka za kihistoria ya Uturuki.
Televisheni ya al Mayadeen imemnukuu Mustafa al Barghouthi akisema hayo jana na kuongeza kuwa, utawala wa Kizayuni hauna chembe ya utu kiasi kwamba, haukuona hata haya kuiba nyaraka muhimu za nchi iliyokumbwa na janga kubwa la kimaumbile kama ilivyotokea hivi sasa kwa nchi mbili za Uturuki na Syria. Amesema, nyaraka hizo zinahusiana na matukio ya miaka 200 au 300 nyuma na zilikuwa zimefukiwa kwenye vifusi vya majengo yaliyoporomoka.
Mitetemeko miwili mikubwa ya ardhi ambayo wa kwanza ulikuwa na ukubwa wa 7.8 kwa kipimo cha rishta yaliyakumba maeneo ya mpakani mwa Syria na Uturuki Jumatatu ya wiki iliyopita na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa. Hasara iliyosababishwa na matetemeko hayo ni kubwa kiasi kwamba hadi hivi sasa hakujatolewa takwimu hasa ya hasara hiyo.
Katibu Mkuu wa Harakati ya Ubunifu wa Kitaifa ya Palestina, Mustafa al Barghouthi vile vile amesema, ukatili, jeuri, upofu na kukosa utu Wazayuni ni kukubwa kiasi kwamba, katika mazingira ya huzuni na majonzi kama ya hivi sasa, imewaongezea majanga wananchi wa Syria kwa kufanya mashambulizi ya kikatili kwenye viunga vya Damascus na kuua na kujeruhi watu chungu nzima wasio na hatia.
Shambulio la alfajiri ya jana Jumapili lililofanywa na utawala wa Kizayuni dhidi ya Syria linathibitisha kuwa, kwa mtazamo wa utawala huo dhalimu, maafa ya kibinadamu ni fursa ya kutimiza malengo yake ya kihalifu. La ajabu na la kusikitisha ni kwamba, Jamii ya Kimataifa inaendelea kunyamazia kimya jinai na unyama huo wa Wazayuni.