-
Takriban watu 1,400 wametiwa mbaroni huku maandamano yakiendelea Uturuki licha ya kupigwa marufuku
Mar 26, 2025 07:54Mamlaha husika nchini Uturuki zimewatia mbaroni waandamanaji zaidi ya 1,400 huku maandamano ya mitaani yakiendelea kushuhudiwa katika miji mikubwa ya nchi hiyo kupinga marufuku ya kuandamana kufuatia kufungwa jela Meya wa mji wa Istanbul, Ekrem Imamoglu kwa tuhuma za ufisadi, kuongoza genge la uhalifu, utovu wa nidhamu na mengineyo.
-
Maandamano yarindima Meya wa Istanbul, hasimu wa Rais wa Uturuki alipokamatwa
Mar 20, 2025 03:09Maelfu ya wananchi wa Uturuki wamemiminika barabarani kulalamikiwa kutiwa mbaroni Meya wa Istanbul, Ekrem Imamoglu, mpinzani mkuu wa kisiasa wa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ambaye amekamatwa kwa tuhuma za rushwa na ugaidi; siku chache kabla ya kuteuliwa kuwa mgombea wa urais.
-
Iran: Machafuko nchini Syria ni kwa manufaa ya Israel
Mar 09, 2025 06:47Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, machafuko na ukosefu wa utulivu nchini Syria ni kwa manufaa ya utawala wa Kizayuni na kwamba magenge ya kigaidi na yenye misimamo mikali yanatumia vibaya fursa hiyo kwa manufaa yao binafsi.
-
Nyaraka zavuja kuhusu msaada wa mafuta wa Erdogan kwa utawala wa Israel
Jan 21, 2025 11:26Mbunge wa Uturuki amewasilisha picha za satalaiti na nyaraka za data za baharini katika bunge la nchi hiyo zinazothibitisha kwamba Ankara imekuwa ikitoa msaada wa mafuta kwa utawala wa Israel.
-
Makundi yanayopigana kwa niaba ya US na Uturuki nchini Syria yatwangana, zaidi ya 100 wauawa
Jan 06, 2025 03:06Wanamgambo zaidi ya 100 wameuawa katika muda wa siku mbili zilizopita kaskazini mwa Syria katika mapigano kati ya makundi yanayoungwa mkono na Uturuki na vikosi vya Wakurdi vinavyoungwa mkono na Marekani. Hayo ni kwa mujibu wa kundi linalofuatilia habari za vita lenye makao yake London, Uingereza.
-
Pezeshkian amwambia Erdogan: Unyakuzi wa ardhi ya Syria haukubaliki kwa njia yoyote
Dec 20, 2024 07:59Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza ulazima wa kuhifadhiwa ardhi yote ya Syria. Rais Masoud Pezeshkian ameyasema hayo katika mazungumzo yake na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki pambizoni mwa mkutano wa viongozi wa nchi wanachama katika D-8 uliofanyika jana mjini Cairo huko Misri.
-
Iran, Russia na Uturuki zalaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina
Nov 13, 2024 02:20Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Russia na Uturuki zimetoa taarifa ya pamoja zikilaani jinai za Wazayuni dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi ya utawala huo ghasibu dhidi ya Lebanon na Syria.
-
Iran: Tunao uwezo wa kuishambulia Israel kwa 'darzeni' za operesheni sawa na "Ahadi ya Kweli"
Oct 30, 2024 13:34Waziri wa Ulinzi Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema Iran inao uwezo wa kuteketeza 'darzeni' za operesheni za kulipiza kisasi sawa na "Operesheni ya Ahadi ya Kweli" iliyotekeleza mwezi Aprili kulenga maeneo ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Palestina unayoikalia kwa mabavu.
-
Iran yalaani vikali shambulio la kigaidi kwenye makao ya Shirika la Anga la Uturuki
Oct 24, 2024 07:28Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani vikali shambulio la kigaidi kwenye makao makuu ya Shirika la Anga la Uturuki (TOSASH) mjini Ankara.
-
Maandamano makubwa ya wananchi wa Jordan na Uturuki kulaani jinai za Israel Gaza
Oct 18, 2024 07:53Maelfu ya wananchi wa Jordan na Uturuki wameandamana na kulaani jinai za utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza.