-
Uvurundo wa karne katika soka
Jul 12, 2016 08:08Hata makosa nayo yanazidiana. Kuna baadhi ya makosa ni "blanda" na uvurundo ambao hufanyika kiutaalamu kiasi kwamba hata aliyefanya uvurundo huo akiambiwa aurudie hawezi kama vinavyoonesha baadhi ya vipande hivi vya sekundi za hatari katika soka...
-
Mtu hafi ila kwa siku yake kufika
Jul 12, 2016 08:05Kuna matukio mbalimbali hutokezea katika maisha ya wanadamu na kuthibitisha kuwa mtu hufa kwa ahadi yake kufika. Moja ya matukio hayo ni la dereva huyu aliyenusurika kifo kwa sekunde chache tu.
-
Utamu wa kabumbu... Pasi za ajabu katika kandanda... Utafurahi
Jul 04, 2016 09:11Kila mchezo una mvuto wake, lakini kwa mashabiki wa kandanda, watakubaliana nami kuwa, mvuto ulioomo kwenye kipande hiki cha video hawajawahi kuona mfano wake... Pasi ipi imekuvutia zaidi? Nina yakini utashindwa kujua ipi imekumaliza zaidi... Ajabu ni kuwa pasi hizo zimetolewa kwenye michuano migumu, si katika mazoezi...
-
Vijana wa Lamu Kenya wafanya usafi kujitayarisha kwa sikukuu ya Idul Fitr
Jul 02, 2016 12:51Vijana wa Lamu nchini Kenya wameendeleza sunna nzuri ya kufanya usafi kwa ajili ya kujitayarisha kwa sikukuu kubwa ya Waislamu, sikukuu ya Idul Fitr. Video hii inaonesha baadhi ya vijana hao wakiwa kazini wakizungumzia suala hilo...
-
Baadhi ya wakati wanyama wanawazidi binadamu kwa kuoneana huruma
Jul 02, 2016 10:05Baadhi ya wakati wanyama huoneana huruma kuliko hata wanadamu, kama wanavyoonesha makobe hawa wawili katika kipande hiki cha video kilichoenea kwenye mitandao ya kijamii.
-
Mchezo mwingine wa kucheza na roho za watu haufai...
Jul 02, 2016 09:57Rubani wa ndege hii, bila ya kujali idadi kubwa ya roho za watu zilizoko kwenye dhima yake, alifanya mchezo huu wakati akirusha ndege. Michezo ya namna hii haifai...
-
Jeshi la Iraq liliposhambulia msafara mkubwa wa Daesh nje ya Fallujah
Jul 02, 2016 09:10Baada ya kuzidiwa nguvu katika mji muhimu na wa kiistratijia wa Fallujah nchini Iraq, kundi la Daesh (ISIS) liliamua kukimbia kwenye msafara mkubwa wa magari kuelekea upande wa Syria kwa ajili ya kuunganisha nguvu upya. Hata hivyo jeshi la anga la Iraq liliushambulia vikali msafara huo wa Daesh kama inavyoonesha video hii kutoka Wizara ya Ulinzi ya Iraq.
-
Ngedere akionyesha manjonjo yake juu ya "kapikipiki"
Jun 29, 2016 07:59Uvundi wa kuendesha pikipiki hauishii kwa wanadamu tu, hata wanyama wanaweza, kama anavyothibitisha kima huyu anayeonesha manjonjo ya aina yake anapokuwa juu ya "kapikipiki." Ajabu ni kuwa anajua hela kweli! Akitunzwa anatua pikipiki anakusanya fedha anatia kwenye kihelmeti chake halafu anaendelea na kuonyesha manjonjo yake...
-
Maajabu ya kandanda hayana mwisho, huwezi kuamini...
Jun 29, 2016 07:54Kandanda yaani soka ina maajabu mengi; ona maajabu yake katika penati, huwezi kuamini kama ni kweli hadi ujionee mwenyewe kwenye video hii....
-
Basi la shule
Jun 28, 2016 06:21Duniani kuna maajabu, hili ni moja ya maajabu hayo...