-
Ripoti: Watu 350,000 wamekumbwa na baa la njaa huko Tigray nchini Ethiopia
Jun 10, 2021 21:43Kamati ya ngazi ya juu inayoongozwa na UN ambayo inajihusisha na kutafuta majibu ya haraka kwa mizozo ya kibinadamu inakadiria kwamba, karibu watu 350,000 katika mkoa wa Tigray uliokumbwa na vita huko Ethiopia wanasumbuliwa na baa la njaa.
-
Baraza la Haki za Binadamu la UN leo linajadili mpango wa kuundwa tume ya kuchunguza jinai za Israel dhidi ya Wapalestina
May 26, 2021 21:49Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limepokea muswada unaotaka kuundwa tume ya kimataifa itakayochunguza jinai na uhalifu uliofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.
-
Baraza la utawala wa kijeshi Chad latangaza ushindi dhidi ya waasi wa FACT
May 10, 2021 08:06Jeshi la Chad limejitangazia ushindi dhidi ya waasi kufuatia mapigano ya wiki kadhaa yaliyosababisha kifo cha Rais wa muda mrefu wa nchi hiyo, Idriss Deby kwenye uwanja wa vita.
-
Viongozi wa Somalia washindwa kukubaliana juu ya ajenda ya mkutano muhimu wa uchaguzi
Apr 05, 2021 08:24Viongozi wa Somalia wameshindwa kufikia makubaliano juu ya ajenda kuu ya mkutano muhimu wa uchaguzi, suala ambalo limedhihirisha tena ufa uliopo kati ya makundi ya kisiasa ya Somalia.
-
Wanafikra Wazayuni: Israel ni dhaifu na tete katika kukabiliana na vita vya pande zote
Apr 02, 2021 23:04Kituo cha tafiti za usalama wa ndani cha utawala haramu wa Kizayuni wa Israel kimesema, hatari kuu inayokabili uwepo wa utawala huo ni vita vya pande zote kutokea kaskazini, mashariki na kusini.
-
Mabilioni ya dola yapotea katika vita vya Marekani huko Afghanistan
Mar 01, 2021 08:44Wasimamizi wa serikali ya Marekani wametoa ripoti na kukiri juu ya kupotea mabilioni ya dola fedha zilizotumika katika vita vya miaka 20 vya nchi hiyo huko Afghanistan.
-
Taliban yaonya kuwa itaanzisha tena vita kamili dhidi ya Marekani nchini Afghanistan
Feb 27, 2021 03:01Msemaji wa Taliban amesema, kundi hilo halitakubali kuangaliwa upya au kufanywa mazungumzo tena kuhusu mapatano ya Qatar iliyofikia Marekani; na endapo Marekani itayakiuka mapatano hayo, huo utakuwa ni uanzishaji wa vita vipya nchini Afghanistan.
-
Kukataa kuomba radhi Macron kwa jinai ilizofanya Ufaransa enzi za ukoloni nchini Algeria
Jan 22, 2021 06:55Ufaransa, ambayo ilikuwa moja ya madola ya kikoloni, ina faili chafu na la kuaibisha kuhusiana na uvamizi, ukaliaji ardhi kwa mabavu na vitendo vya jinai ilivyofanya mnamo karne ya 20 katika nchi ilizozikoloni hususan Algeria.
-
Walibya wavamia makazi ya kijeshi ya Haftar, wataka kulipiza kisasi dhidi ya mamluki
Jan 01, 2021 09:55Wakazi wa mji wa Houn katika eneo la al Jufra huko katikati mwa Libya wamefanya maandamano wakitaka kulipiza kisasi kwa mamluki wa kampuni ya Wagner ya Russia na wapiganaji wa kundi la Janjaweed kutoka Sudan wanaolisaidia jeshi la jenerali muasi, Khalifa Haftar baada ya mauaji ya raia kadhaa wa eneo hilo.
-
Kuendelea mgogoro wa Tigray nchini Ethiopia na hatari zake
Nov 23, 2020 09:03Mgogoro katika jimbo la Tigray nchini Ethiopia umechukua muelekeo mpya ambapo Abiy Ahmed, Waziri Mkuu wa nchi hiyo amewapa viongozi wa jimbo hilo muda wa masaa 72 wawe wamejisalimisha na kuweka chini silaha zao, la sivyo, atazingira na kuyashambulia makao makuu ya eneo hilo.