-
Sisitizo la Iran la kurudishwa amani ya kudumu katika eneo kwa kuondolewa ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina
Apr 22, 2022 08:16Hussein Amir Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa amani ya kudumu katika eneo la Asia Magharibi itapatikana tu kwa kuondolewa kikamilifu ukaliwaji mabavu wa ardhi za Palestina, kurejea wakimbizi wote katika ardhi zao za jadi na kuainishwa mfumo wa utawala wa baadaye wa Palestina kwa msingi wa kura ya maoni pamoja na kuundwa serikali huru katika ardhi hizo.
-
Safari ya Lavrov nchini India na sisitizo la kutumiwa sarafu ya Ruble katika biashara
Apr 03, 2022 07:03Sergey Viktorovich Lavrov, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amefanya ziara ya siku mbili ya kuitembelea kikazi India na kuonana na waziri mwenzake wa nchi hiyo Subrah Jaishankar na waziri mkuu wa India Narendra Modi.
-
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Iran na China Wasisitiza Udharura wa Kukabiliana na Vikwazo Haramu
Apr 02, 2022 08:15Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Hossein Amir-Abdollahian na mwenzake wa China, Wang Yi wamejadili masuala ya pande mbili, kieneo na kimataifa pembezoni mwa mkutano wa tatu wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi jirani na Afghanistan.
-
Shutuma za Russia kwa Marekani inayokwamisha mazungumzo ya Ukraine
Mar 22, 2022 02:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergeĭ Viktorovich Lavrov ameishutumu vikali Marekani kwa siasa zake kuhusu vita vya Ukraine na kusema kuwa, Washington ndiyo inayokwamisha kufikiwa makubaliano baina ya Moscow na Kyiv hata katika masuala madogo kabisa. Amesema, hivi sasa Marekani inawatwisha viongozi wa Ukraine misimamo yake na ndio maana Kyiv inakwamisha kila kitu katika mazungumzo yake na Russia.
-
Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran nchini Russia na matokeo yake
Mar 17, 2022 06:38Hossein Amir-Abdollahian, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran aliwasili mjini Moscow siku ya Jumanne akiongoza ujumbe wa ngazi za juu kwa ajili ya kukutana na kuzungumza na Sergey Lavrov, Waziri mwenzake wa Mambo ya Nje wa Russia kuhusu masuala ya pande mbili, mazungumzo ya Vienna, Ukraine, Syria, Yemen na Afghanistan.
-
Feisal Miqdad: NATO imevuruga uthabiti wa dunia
Mar 03, 2022 00:05Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema Russia ina haki ya kuchukua hatua za kukabiliana na sera za NATO kujipenyeza ukanda wa mashariki na kuongeza kuwa, NATO sasa imegeuka kuwa hatari kwa dunia. Amesema majeshi ya Russia na Syria yanakabiliwa na tishio la NATO.
-
Kufutiwa utawala ghasibu wa Israel hadhi ya mwanachama mtazamaji katika Umoja wa Afrika
Feb 08, 2022 08:58Mkutano wa 35 wa wakuu wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika tarehe 5 na 6 za mwezi huu wa Februari huko Addis Ababa Ethiopia umesitisha hadhi ya utawala ghasibu wa Israel ya kuwa mwanachama mtazamaji katika umoja huo.
-
Russia yakosoa mwenendo wa kinafiki wa Marekani kuhusu masuala ya anga
Nov 19, 2021 02:53Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amezitaja tuhuma za Marekani dhidi ya Moscow kwamba inatumia silaha dhidi ya satalaiti na kusababisha vitisho angani kuwa ni za kinafiki na zisizo na ukweli wowote. Sergey Lavrov amesema kuwa: "Tunaona kwkamba, badala ya kutoa madai yasiyo na msingi wowote, ni vyema Marekani iketi kwenye meza ya mazungumzo na ieleze mitazamo yake kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa na Russia na China kwa ajili ya kuzuia mashindano ya silaha angani
-
Kushindwa Marekani kuzuia kuanzishwa tena uhusiano wa nchi za Kiarabu na Syria
Oct 16, 2021 07:23Akizungumza Jumatano mbele ya waandishi habari mjini Washington, Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani amesema nchi hiyo haina nia ya kuunga mkono juhudi za kuboreshwa uhusiano na serikali ya Syria.
-
Sudan: Hakuna ishara zozote za kuboreka uhusiano wetu na Israel
Sep 27, 2021 13:00Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan amesema kuwa, miezi 11 imepita tangu nchi yake itangaze kuwa na uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni wa Israel lakini hakuna ishara zozote za kuboreka uhusiano wa pande mbili kama ambavyo hakuna pia mazungumzo yoyote rasmi baina yao.