Feisal Miqdad: NATO imevuruga uthabiti wa dunia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i80952-feisal_miqdad_nato_imevuruga_uthabiti_wa_dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema Russia ina haki ya kuchukua hatua za kukabiliana na sera za NATO kujipenyeza ukanda wa mashariki na kuongeza kuwa, NATO sasa imegeuka kuwa hatari kwa dunia. Amesema majeshi ya Russia na Syria yanakabiliwa na tishio la NATO.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Mar 02, 2022 20:35 UTC
  • Feisal Miqdad: NATO imevuruga uthabiti wa dunia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria amesema Russia ina haki ya kuchukua hatua za kukabiliana na sera za NATO kujipenyeza ukanda wa mashariki na kuongeza kuwa, NATO sasa imegeuka kuwa hatari kwa dunia. Amesema majeshi ya Russia na Syria yanakabiliwa na tishio la NATO.

Feisal Miqdad, Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria ameyasema hayo Jumatano ambapo ametangaza kuwa nchi yake inaunga mkono Russia. Aidha amesema, muungano wa kijeshi wa NATO unahatarisha usalama wa dunia na umeanzisha mashindano ya silaha na hivyo kupelekea kuwepo uwezekano wa kuanza vita vikubwa vikiwemo vita vya nyuklia.

Halikadhalika amesema Syria inalaani  Marekani na waitifaki wake kwa kuanzisha mgogoro  wa Ukraine kwa lengo la kuhatarisha usalama wa Russia.

Feisal Miqdad amesisitiza kwa mara nyingine kuhusu kuunga mkono mazungumzo ya Kongamano la Kuweka Chini Silaha kwa msingi wa rasimu ya mapatano ya kuzuia ugaidi wa silaha za sumu. 

Baada ya viongozi wa eneo la Donbas ambalo limetangaza kujitenga na Ukraine kuiomba Russia iwatumie misaada ya kijeshi kulingana na mikataba ya ushirikiano iliyoko baina yao, siku ya Alkhamisi ya tarehe 24 Februari, Rais Vladimir Putin wa Russia alitangaza katika hotuba aliyotoa kupitia televisheni  ya nchi hiyo kuanza kwa operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbas.

Hivi sasa Russia inaendelea kuandamwa na vikwazo vikali vya Marekani na waitifaki wake kwa sababu ya kuwaunga mkono Waukraine wenye asili ya Russia wa mashariki ya Ukraine na kuunga mkono uamuzi wa maeneo ya Donetsk na Luhansk kutangaza kujitenga na Ukraine..