-
Wakimbizi wa Rwanda zaidi ya 500 warejea nchini kutoka Kongo
Aug 25, 2025 23:19Wakimbizi wa Kinyarwanda zaidi ya 500 jana Jumatatu walirejea nyumbani wakitokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Kampuni ya Mafuta ya Serikali ya Nigeria: Wizi wa mafuta kupitia mabomba wakaribia kukomeshwa
Aug 25, 2025 23:15Kampuni ya mafuta ya serikali ya Nigeria (NNPC Limited) imeripoti kuwa karibu wizi wote wa mafuta uliokuwa ukifanywa kupitia mabomba umekaribia kukomeshwa, baada ya juhudi zilizoratibiwa na mashirika ya ulinzi na intelijensia ya nchi hiyo.
-
Raia 13 wauawa na wanamgambo wa RSF huko Darfur, Sudan
Aug 25, 2025 07:04Raia wasiopungua 13 wa Sudan wameripotiwa kuuawa na wapiganaji wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) huko Darfur Kaskazini.
-
Jeshi la Nigeria laokoa watu 76 waliokuwa wametekwa nyara, wamo wanawake na watoto
Aug 25, 2025 03:29Maafisa wa serikali ya Nigeria wamesema, jeshi la anga limeokoa watu 76 waliokuwa wametekwa nyara, wakiwemo wanawake na watoto.
-
Je, ushirikiano wa kijeshi wa Marekani na Nigeria unaongeza hatari ya ukiukaji wa haki za binadamu?
Aug 25, 2025 02:23Hivi karibuni Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kuwa ili kuisaidia Nigeria katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi, imekubali kuiuzia nchi hiyo silaha zenye thamani ya takriban dola milioni 346.
-
Wanahabari wa Afrika waunda Muungano wa Kupinga Mauaji ya Kimbari ya Israel Gaza
Aug 24, 2025 23:29Waandishi wa habari kutoka bara zima la Afrika wamezindua muungano uliopewa jina la 'African Journalists Against Genocide (AJAG)' wenye lengo la kupinga kile wanachoeleza kuwa ni mauaji ya kimbari ya Israel na uhalifu wa kivita dhidi ya watu wa Gaza, wakiwemo wanahabari wenzao.
-
TICAD inaimarisha vipi nafasi ya Afrika katika siasa na uchumi wa dunia?
Aug 24, 2025 23:01Mkutano wa 9 wa Kimataifa wa Maendeleo ya Afrika, Tokyo International Conference on African Development (TICAD), ulimalizika Ijumaa, Agosti 22 kwa kusainiwa mikataba takriban 300 ya ushirikiano kati ya taasisi za Japan na Afrika kuhusu masuala mbalimbali ya afya, teknolojia, elimu, kilimo, maendeleo ya miundombinu na ujenzi wa miundomsingi.
-
Serikali ya Eswatini inakabiliwa na kesi mahakamani kuhusu watu waliofukuzwa Marekani
Aug 24, 2025 07:24Kundi la mawakili watetezi wa haki za binadamu na taasisi zisizo na kiserikali (NGOs) linaishtaki serikali ya Eswatini kwa kukubali kuwapa hifadhi watu watano waliofukuzwa nchini Marekani.
-
Watu 46 wapoteza maisha kutokana na njaa katika jimbo la Kordofan nchini Sudan
Aug 24, 2025 04:30Angalau watu 46, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, wamefariki kutokana na njaa nchini Sudan katika jimbo la Kordofan Kusini katika kipindi cha miezi miwili iliyopita. Hayo yamedokezwa na Shirika la Madaktari wa Sudan huku eneo hilo lenye vita likikumbwa na njaa kali na uhaba wa dawa.
-
Chanjo kutoka Afrika: Matumaini yapatikana
Aug 23, 2025 23:25Tangu janga la Corona (UVIKO-19), Afrika imezindua mipango ya kutengeneza chanjo na dawa kwa ajili ya kuboresha huduma za afya. Ingawa mafanikio ya awali yanaonekana, lakini bado kunahitajika ufadhili wa muda mrefu.