-
ANC yamkosoa Mfalme wa Afrika Kusini kwa kuwaalika maafisa wa Israel
Feb 04, 2026 06:53Chama tawala cha African National Congress (ANC) kimemkosoa vikali Mfalme wa Afrika Kusini, Buyelekhaya Dalindyebo kufuatia uamuzi wake tata wa kuwaalika maafisa kutoka Ubalozi wa Israel kutembelea hospitali za umma katika mkoa wa Eastern Cape. Dalindyebo ni mfalme wa watu wa AbaThembu, mojawapo ya jamii kubwa zaidi za kitamaduni za Afrika Kusini.
-
Mashambulizi ya droni yaua watu 15 Kadugli, kusini mwa Sudan
Feb 04, 2026 06:52Raia wasiopungua 15, wakiwemo watoto saba, wameuawa katika mashambulizi ya ndege zisizo na rubani katika mji wa Kadugli kusini mwa Sudan. Hayo yamesemwa na kundi la kujitolea la wenyeji na mashuhuda wa hujuma hiyo ambao wameeleza kuwa, mashambulizi hayo yamejiri saa chache baada ya jeshi la Sudan kutangaza kuvunja mzingiro wa miaka mingi dhidi ya mji wa Kadugli.
-
Ghannouchi akataa kukata rufaa ya kifungo cha miaka 20 jela kutokana na "ukosefu wa dhamana ya haki"
Feb 04, 2026 03:51Rached Ghannouchi, mkuu wa harakati ya Ennahda na spika wa zamani wa Bunge la Tunisia, alitangaza jana Jumanne kwamba hatakata rufaa mahakamani dhidi ya hukumu ya kifungo cha miaka 20 jela aliyokatiwa katika kile kinachojulikana katika vyombo vya habari kama "Kesi ya Kula Njama - 2," akisema kwamba kesi hiyo haina dhamana ya haki.
-
Abiy Ahmed: Ethiopia kuzindua chuo kikuu cha pili duniani cha AI mwaka 2027
Feb 04, 2026 03:48Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, jana alieleza kuwa Chuo Kikuu cha pili duniani kilichojikita katika akili mnemba (AI) kinatarajiwa kuzinduliwa nchini Ethiopia mwaka kesho wa 2027.
-
Makomando 4 walizima kamera na kumpiga risasi... Maelezo mapya yaibuka kuhusu mauaji ya Saif al-Islam Gaddafi
Feb 03, 2026 23:56Timu ya kisiasa ya Saif al-Islam Gaddafi, mtoto wa kiume wa kiongozi wa zamani wa Libya, Muammar Gaddafi, imefichua kwamba mauaji yake yamefanywa na watu wanne wasiojulikana waliokuwa na silaha, ambao walivamia nyumba yake katika mji wa Zintan (kilomita 200 kusini-magharibi mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli) alasiri ya jana Jumanne.
-
Ethiopia yakanusha madai ya Trump kuwa Marekani ilifadhili mradi wa Bwawa la Renaissance
Feb 03, 2026 23:46Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amesema kuwa nchi hiyo haikupokea “hata senti moja” kutoka kwa serikali yoyote ya kigeni kwa ajili ya kufadhili ujenzi wa Bwawa Kuu la Renaissance la Ethiopia (GERD), akikanusha madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kwamba Marekani imefadhili mradi huo.
-
Jeshi la Sudan lapata mafanikio katika vita dhidi ya waasi wa RSF
Feb 03, 2026 23:40Jeshi la Sudan limevunja mzingiro uliowekwa na waasi dhidi ya mji muhimu wa Kusini, Kadugli, Jumanne. Hayo yametangazwa na Rais wa mpito na Mkuu wa Jeshi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.
-
Umoja wa Mataifa kutuma ujumbe wa kusimamia usitishaji mapigano nchini Congo DR
Feb 03, 2026 07:15Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kwamba ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Congo utatuma timu yake ya kwanza kusimamia usitishaji mapigano kati ya serikali na muungano wa "Mto Kongo", (Alliance Fleuve Congo) kwa Kifaransa, unaojumuisha harakati ya M-23, katika siku zijazo.
-
Wakenya waendelea kujiunga na vita Ukraine licha ya maafa yanayowapata
Feb 03, 2026 06:48Uchunguzi umebaini kuwa baadhi ya Wakenya wanaopigana katika vita vinavyoendelea huko Ukraine waliajiriwa kupitia maombi ya moja kwa moja na kampuni moja ya nchini Kenya, ambapo walitakiwa kurekodi video wakieleza nia yao ya kuajiriwa kama wanajeshi.
-
Nigeria yawafungulia mashtaka watu 9 kwa mauaji ya watu 150 mwaka jana huko Yelwata
Feb 03, 2026 04:37Waendesha mashtaka wamewafungulia mashtaka watu tisa kwa makosa ya ugaidi kuhusiana na moja ya mauaji mabaya zaidi yaliyojiri jimbo la Benue mnamo mwezi Juni mwaka jana. Mauaji hayo yalilenga pakubwa jamii ya Yelwata.