-
Misri: Tunatumai mazungumzo ya Iran na Marekani yatasaidia kupunguza mivutano
Apr 13, 2025 07:04Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imetangaza kuwa inatarajiwa mazungumzo kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Marekani yataanzisha awamu mpya itakayosaidia kuimarisha amani na kupunguza mivutano katika eneo la Magharibi mwa Asia kwa ujumla hususan Ukanda wa Gaza.
-
Mamia wauawa na kujeruhiwa katika shambulio la RSF kwenye kambi ya Zamzam
Apr 13, 2025 03:24Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan na mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema kuwa mamia ya watu wameuawa na kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa jana na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) kwenye kambi ya Zamzam ya wakimbizi wa ndani katika mji wa El Fasher, Jimbo la Darfur Kaskazini, magharibi mwa Sudan.
-
Côte d'Ivoire yaatishia kuongeza gharama za mauzo ya kakao katika kukabiliana na ushuru wa Trump
Apr 13, 2025 02:55Waziri wa Kilimo wa Côte d'Ivoire, Kobenan Kouassi Adjoumani, amesema nchi yake, mzalishaji mkubwa wa kakao duniani, inaweza kuchukua hatua ya kuongeza bei ya bidhaa hiyo iwapo mapendekezo ya ushuru wa Rais Donald Trump wa marekani dhidi ya nchi yake yataanza kutekelezwa.
-
Ni rasmi, CHADEMA haitaruhusiwa kushiriki uchaguzi ujao Tanzania
Apr 12, 2025 09:34Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC), Ramadhani Kailima, amesema Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) hakitaruhusiwa kushiriki Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu, pamoja na chaguzi zote ndogo zitakazofanyika kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
-
Sudan: RSF imeua raia wengine 32 El-Fasher, Darfur Kaskazini
Apr 12, 2025 08:09Jeshi la Sudan limesema kwa uchache raia 32 wameuawa katika shambulio jipya la Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) huko El-Fasher, makao makuu ya Jimbo la Darfur Kaskazini.
-
Wanawake na watoto, wahanga wakuu wa unyanyasaji wa kingono DRC
Apr 12, 2025 03:05Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) limesema katika ripoti yake ya karibuni kabisa iliyotolewa jana Ijumaa kwamba, kwa wastani kila baada ya dakika 30 mtoto mmoja alibakwa wakati wa mapigano makali ya Januari na Februari huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Gabon wafanya uchaguzi leo; ni wa kwanza baada ya mapinduzi ya kijeshi
Apr 12, 2025 03:05Wananchi wa Gabon leo Jumamosi wanashiriki kwenye uchaguzi wake wa kwanza wa rais tangu yalipotokea mapinduzi ya kijeshi yaliyomaliza utawala wa miaka 56 ya familia ya Bongo, na kuweka mazingira ya kurejea kwenye utawala wa kiraia katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati.
-
UN: Katika kila nusu saa, mtoto 1 alibakwa mashariki ya DRC
Apr 11, 2025 22:49Umoja wa Mataifa umelaani kushtadi kesi za ubakaji na unyanyasaji wa kingono dhidi ya watoto huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zilizoripotiwa katika miezi miwili ya kwanza ya mwaka huu; huku makabiliano makali yakiendelea kati ya kundi la waasi la M23 na vikosi vya serikali.
-
Asasi za kiraia, wapinzani Tanzania walaani kukamatwa Tundu Lissu
Apr 11, 2025 09:02Mashirika ya kiraia, vyama vya upinzani na asasi za kutetea haki za binadamu nchini Tanzania zimekosoa vikali hatua ya kukamatwa na kushtakiwa Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini humo CHADEMA.
-
Afrika Kusini yatoa mwito wa kuimarishwa mfumo wa biashara wa pande nyingi kuikabili Marekani
Apr 11, 2025 07:27Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametoa mwito kwa jamii ya kimataifa kuimarisha mfumo wa biashara wa pande nyingi ambao hivi sasa unatishiwa na siasa za kibeberu za Marekani.