-
Afrika Kusini imeanza kuwaondoa chini ya ardhi wanaochimba madini kinyume cha sheria
Nov 20, 2024 08:18Wataalamu wa uokoaji wa Afrika Kusini wamefika katika mgodi wa Stilfontein nchini humo kuanza operesheni ya kuwatoa chini ya ardhi wachimba madini kinyume cha sheria.
-
Al-Burhan: Vita vinakaribia kuisha na hakuna mapatano na maadui wa taifa
Nov 20, 2024 04:37Mkuu wa Baraza la Utawala wa Mpito nchini Sudan, Abdel Fattah Al-Burhan, amesema wakati wa mkutano wa kiuchumi katika mji wa Port Sudan kwenye pwani ya Bahari Nyekundu kwamba vita na kundi la RSF inakaribia mwisho, ikisisitiza kwamba hakuna nafasi ya mazungumzo na mapatano na kile alichokiita “maadui wa taifa.”
-
Spika wa Bunge Kenya asema: Wabunge mtasafiri kwa treni, si kwa ndege, tunabana matumizi
Nov 20, 2024 04:35Spika wa Bunge la Kenya amesema wabunge watakaoshiriki katika michezo baina ya wabunge wa mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA), watasafiri kwenda Mombasa kwa gari moshi sio kwa ndege kama ilivyozoeleka.
-
Femi Fani Kayode: Mataifa ya Afrika yanapaswaa kuvunja uhusiano na Israel
Nov 19, 2024 23:08Waziri wa zamani wa Usafiri wa Anga nchini Nigeria na kiongozi wa Kikristo nchini humo amezitaka nchi za Kiafrika kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na utawala ghasibu wa Israel ili kuwashinikiza Wazayuni wakomeshe mauaji ya kimbari dhidi ya watu wa Palestina na Lebanon.
-
Polisi wa Afrika Kusini wanapanga kuwaondoa wachimba madini haramu chini ya ardhi
Nov 19, 2024 23:07Msemaji wa Polisi ya Afrika Kusini, Athlenda Mathe, amesema kuwa wataalamu wa uokoaji wamekutana ili kutekeleza operesheni ya kuwatafuta wachimbaji haramu katika mgodi uliotelekezwa. Haya yanajiri huku kukiwa na mzozo kati ya wachimba migodi na polisi ya Afrika Kusini ambao umeendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa.
-
Siku ya Utamaduni wa Washirazi yaadhimishwa nchini Tanzania
Nov 19, 2024 07:42Balozi wa Iran nchini Tanzania ameshiriki katika Siku ya Utamaduni wa Washirazi iliyofanyika jijini Dar es Salaam ili kuzidi kutia nguvu uhusiano wa kiudugu ulipo baina ya Iran na Tanzania.
-
Wahamiaji 604 walizuiwa kuendelea na safari kwenye pwani ya Libya wiki iliyopita
Nov 19, 2024 07:40Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa, wahamiaji 604 walikamatwa na kurudishwa nje ya pwani ya Libya wiki moja iliyopita wakati walipokuwa wanahatarisha maisha yao kujaribu kuelekea barani Ulaya kwa kutumia vyombo dhaifu mno vya baharini.
-
Watu 3 wauawa katika shambulizi la wanaotaka kujitenga nchini Cameroon
Nov 19, 2024 07:19Takriban watu watatu yaani mwanajeshi mmoja na raia wawili wameuawa katika shambulio la watu wanaotaka kujitenga kwenye eneo linalotokea vita vya mara kwa mara la kaskazini magharibi mwa Cameroon.
-
Waziri Tuggar: Nigeria inaunga mkono juhudi za ukombozi wa Palestina
Nov 18, 2024 23:11Yusuf Maitama Tuggar, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Nigeria amesema kuwa nchi yake ingali inaunga mkono juhudi za kisiasa na kiuchumi za ukombozi wa Palestina.
-
Wananchi wa Gabon wapasisha katiba mpya kupitia kura ya maoni
Nov 18, 2024 23:11Wananchi wa Gabon wamepasisha katiba mpya ya nchi hiyo kwa wingi wa kura katika zoezi la kura ya maoni lililofanyika Jumamosi iliyopita.