-
Jeshi la Sudan: Tumeua wapiganaji 150 wa RSF Magharibi mwa nchi
Nov 18, 2024 06:41Jeshi la Sudan (SAF) limetangaza kwamba limeua wapiganaji 150 wa Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) katika vita vilivyozuka baina ya pande hizo mbili, huko El Fasher, makao makuu ya jimbo la Darfur Kaskazini la magharibi mwa Sudan.
-
Rais Samia: Tumepoteza wenzetu 13 Kariakoo
Nov 18, 2024 00:00Watu 13 wamethibitika kufariki dunia na wengine 84 kujeruhiwa kufuatia ajali ya kuporomoka kwa jengo katika eneo la Kariakoo mkoani Dar es Salaam, iliyotokea juzi Jumamosi Novemba 16.
-
Mamilioni ya Wasenegal wameelekea vituo vya kupigia kura kuchagua Bunge jipya
Nov 17, 2024 08:43Wasenegal leo wamepiga kura katika uchaguzi wa Bunge ambao utaamua kama rais mpya wa nchi hiyo Bassirou Diomaye Faye ataweza kufanya mageuzi makubwa aliyokusudia au la.
-
Jenerali wa Nigeria: Magaidi, waasi barani Afrika wanatumia silaha za Israel
Nov 17, 2024 04:31Jenerali mstaafu wa jeshi la Nigeria ambaye alikwenda katika nchi kadhaa za Afrika zikiwemo Mali na Liberia kwa ajili ya kulinda amani, amefichua kuwa silaha nyingi walizozikamata kutoka kwa magaidi na waasi wa nchi tofauti zinatoka Israel, jambo ambalo limeweka wazi mkono wa Wazayuni katika migogoro na ugaidi unaotokea katika baadhi ya nchi za Afrika.
-
Waandishi habari Sudan wanatangatanga, vita vimewalazimisha wengine kuacha kazi
Nov 17, 2024 04:19Baada ya vita vya zaidi ya miezi 18 nchini Sudan kati ya jeshi la taifa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF), hali ya wadau wa vyombo vya habari nchini humo imeendelea kuwa mbaya, na wengi wao wamepoteza ajira zao na baadhi yao wamelazimika kuingia kwenye nyanja nyingine kwa ajili ya kutafuta riziki.
-
Tanzania: Watu watano wafariki dunia baada ya jengo kuporomoka Kariakoo
Nov 16, 2024 07:00Watu watano wamefariki dunia, na zaidi ya 40 kujeruhiwa baada ya jengo kuporomoka katika eneo la Kariakoo, Dar es Salaam, nchini Tanzania.
-
Wananchi wa Gabon washiriki kura ya maoni ya marekebisho ya katiba
Nov 16, 2024 10:08Raia wa Gabon wamepiga kura ya maoni ya kuidhinisha katiba mpya katika hatua ambayo inaonekana kuwa muhimu kwa ajili ya kurejesha utawala wa kiraia katika taifa hilo la Afrika ya Kati.
-
Wananchi wa Morocco waandamana kuunga mkono Palestina
Nov 16, 2024 08:54Wananchi wa Morocco wameandamana na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Gaza na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Kwa mara nyingine Ronald Lamola ataka kukomeshwa vita mara moja Ghaza
Nov 16, 2024 03:53Kwa mara nyingine tena, Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini ametaka kukomeshwa vita mara moja katika Ukanda wa Ghaza huko Palestina na kufikishiwa misaada wakazi wa eneo hilo haraka iwezekanavyo.
-
Afrika Kusini yachukua hatua baada ya watoto 22 kufa kwa sumu
Nov 16, 2024 03:52Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameamuru kuondolewa dawa hatari za kuua wadudu barabarani na madukani kama moja ya hatua za kuzuia kuenea sumu ya chakula ambayo iliua watoto 22 hivi karibuni.