-
Nigeria yaripoti vifo 15,000 vinavyohusiana na UKIMWI kila mwaka
Nov 15, 2024 23:23Nigeria inarekodi takriban vifo 15,000 vinavyohusiana na Ugonjwa wa Ukimwi kila mwaka licha ya juhudi za serikali za kukabiliana na kuenea ugonjwa huo hatari katika nchi hiyo yenye watu wengi zaidi barani Afrika.
-
Wasudani elfu 343 wamekimbia makazi yao, 503 wameuawa huko Al-Hilalia
Nov 15, 2024 23:22Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza kuwa mamia kwa maelfu ya watu wamekimbia kutoka Jimbo la Aljazira katikati mwa Sudan na kuhamia maeneo mengine, tangu Oktoba 20, huku idadi ya vifo katika mji wa Hilaliya katika jimbo hilo ikiongezeka hadi watu 503 kutokana na mashambulizi ya Vikosi vya Msaada wa Haraka, (RSF).
-
Afrika Kusini yatangaza maafa ya taifa kutokana na mafuriko na kimbunga
Nov 15, 2024 08:37Serikali ya Afrika Kusini imetangaza hali ya maafa ya taifa zima kufuatia mafuriko makubwa na kimbunga kilichosababisha uharibifu mkubwa wa mali na vifo vya watu katika majimbo saba kati ya tisa ya nchi hiyo.
-
Viongozi wa Jumuiya ya SADC kujadili machafuko ya Msumbiji
Nov 15, 2024 07:45Viongozi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC wanatarajiwa kukutana mwishoni mwa juma hili, katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare kwa minajili ya kujadili mzozo wa Msumbiji.
-
Kaunti 4 za Kenya zinakabiliwa na ukame mkubwa na janga la njaa
Nov 15, 2024 07:38Kaunti nne ambazo ziko kwenye maeneo yanayokumbwa mno na ukame zinakabiliwa na hatari ya janga kubwa la njaa ambalo linaweza kuwatumbukiza takriban watu milioni moja katika hatari ya ukosefu wa chakula nchini Kenya.
-
Watu milioni 7.3 waugua Malaria Ethiopia; 1,157 waaga dunia katika miezi 9
Nov 15, 2024 04:13Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, watu zaidi ya milioni 7.3 wamepatwa na ugonjwa wa Malaria nchini Ethiopia huku wagonjwa 1,157 wakiaga dunia kwa ugonjwa huo kuanzia Januari Mosi hadi Oktoba 20 mwaka huu.
-
Utafiti mpya: Idadi ya waliouawa vitani Sudan inaweza kuwa ya juu zaidi
Nov 15, 2024 00:24Zaidi ya watu 61,000 wanakadiriwa kupoteza maisha katika jimbo la Khartoum katika kipindi cha miezi 14 ya kwanza ya vita vya Sudan. Ushahidi unaonyesha kuwa idadi ya watu waliouliwa vitani ni kubwa zaidi kuliko ilivyosajiliwa hapo awali. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya watafiti nchini Uingereza na Sudan.
-
Waislamu wa Tanzania wamkumbuka na kumuenzi Sayyid Hassan Nasrullah
Nov 14, 2024 07:57Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Tanzania wamefanya kumbukumbu ya Arubaini ya Sayyid Hassan Nasrullah aliyekuwa Katibu Mkuu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon.
-
Amnesty International: Silaha za Ufaransa zinatumika vitani Sudan licha ya vikwazo
Nov 14, 2024 07:40Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International limetangaza kuwa, silaha za Ufaransa zimekuwa zikitumika katika vita vya wenyewe kkwa wenyewe nchini Sudan licha ya vikwazo vya silaha vyya Umoja wa Mataifa.
-
Lugha ya Kiswahili kuwa somo la lazima katika shule za msingi Uganda
Nov 14, 2024 07:39Kituo cha Kitaifa cha Ukuzaji Mtaala (NCDC) nchinin Uganda kimetangaza kuwa lugha ya Kiswahili itaanzishwa kama somo la lazima katika shule za msingi kwa awamu kuanzia mwaka ujao 2025.