-
Maporomoko ya udongo yaua watu 16 magharibi ya Madagascar
Nov 14, 2024 03:35Watu wapatao 16 wamefariki dunia wakati mashua waliyokuwa wakisafiria kupitia mtoni magharibi mwa Madagascar kukumbwa na maporomoko ya udongo. Hayo yameelezwa na mamlaka husika za nchi hiyo jana Jumatano.
-
Mripuko wa bomu wa kando ya barabara waua watu 3 katika mji mkuu wa Somalia
Nov 13, 2024 23:16Askari wawili na raia mmoja wameuawa na wengine watatu wamejeruhiwa katika mripuko wa bomu uliotokea kando ya barabara katika mji mkuu wa Somalia wa Mogadishu jana Jumatano.
-
Boko Haram waua raia wasiopungua 10 nchini Cameroon
Nov 13, 2024 23:15Rais wasiopungua 10 wameuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika shambulizi jipya la genge la kigaidi la Boko Haram nchini Cameroon.
-
UN: Nchi zinazohusika ziache kuzipatia silaha pande zinazopigana nchini Sudan
Nov 13, 2024 08:26Umoja wa Mataifa umesema, kuendelea kuwasambazia silaha askari wa jeshi na wa vikosi vya wanamgambo wanaopigana nchini Sudan ndiko "kunakowezesha kufanyika uchinjaji" na lazima kukomeshwe wakati raia wa nchi hiyo wanaendelea kubeba mzigo mkubwa wa vita.
-
Guterres: Mataifa ya dunia yachukue hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Nov 13, 2024 03:36Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kuwa, kuna ulazima wa kuchukua hatua za utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi ili kuwalinda watu kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kutatua changamoto za ufadhili dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
-
Mahakama ya rufaa ya Mali yakataa ombi la kuwaachia huru baadhi ya wapinzani
Nov 13, 2024 03:35Mahakama ya rufaa katika mji mkuu wa Mali, Bamako jana ilikataa ombi la kuwaachiwa huru mawaziri na wanasiasa 11 waliokuwa wakiukosoa uongozi wa kijeshi nchini humo ambao walitiwa nguvuni mwezi Juni kwa kile kilichotajwa kuwa kula njama dhidi ya utawala wa kijeshi.
-
Serikali ya Niger yalifutia leseni shirika jingine la mkoloni Ufaransa
Nov 13, 2024 03:35Utawala wa kijeshi nchini Niger umetangaza kuwa, umefuta leseni ya shirika lisilo la kiserikali la Acted la Ufaransa kufanya kazi nchini humo, katikati ya mvutano na mkoloni wake huyo wa zamani.
-
Kura ya maoni inatabiri kuwa kiongozi wa upinzani atashinda uchaguzi wa urais nchini Ghana
Nov 12, 2024 22:49Uchunguzi wa maoni iunaonyesha kwamba kiongozi mkuu wa upinzani nchini Ghana, John Dramani Mahama, atashinda uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi ujao wa Desemba, na kumweka mbele ya mpinzani wake mkuu, mgombea wa chama tawala, Mahamudu Bawumia.
-
Polisi Msumbiji yakamata kilo 573 za kokeini katika meli ya India
Nov 12, 2024 22:49Polisi ya Msumbiji imekamata kilo 573 sawa na (pauni 1,263) za dawa za kulevya aina ya kokeini katika meli ya India. Haya yameelezwa na Idara ya Taifa ya Upelelezi ya nchi hiyo.
-
Tunisia yasambaratisha mtandao wa magendo ya binadamu karibu na mji mkuu Tunis
Nov 12, 2024 22:48Walinzi wa Taifa wa Tunisia wametangaza kuwa wamesambaratisha mtandao wa magendo ya binadamu unaohusika na kusafirisha wahamiaji wasio na vibali na wamewatia mbaroni watu watano katika operesheni hiyo.