Guterres: Mataifa ya dunia yachukue hatua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema kuwa, kuna ulazima wa kuchukua hatua za utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi ili kuwalinda watu kutokana na mabadiliko ya tabianchi na kutatua changamoto za ufadhili dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema hayo katika hotuba yake ya ufunguzi kwa Mkutano wa Viongozi wa Dunia wa Utekelezaji wa mabadiliko ya tabianchi, katika ngazi ya mawaziri ya COP29, ambayo ilifunguliwa rasmi jana huko Baku Azerbaijanna kubabainisha kuwa mwaka huu wa 2024 unakaribia kuwa mwaka wa joto zaidi uliowahi kurekodiwa duniani.
Dunia ichukue hatua sasa ya kulipa gharama hizi la sivyo ubinadamu utakuja kulipa gharama hiyo, amesisitiza katibu mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa.
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema katika uchumi wa dunia, misukosuko ya ugavi huongeza gharama kila mahali.
Mavuno hafifu yanaongeza bei ya chakula duniani, nyumba zilizosambaratishwa huongeza malipo yote ya bima.
Amesisitiza kuwa "Hii ni hadithi ya dhuluma inayoweza kuepukika, Tajiri ndiye anayesababisha tatizo, maskini wanalipa gharama kubwa zaidi.”