Ripoti: Ujerumani inaajiri wakimbizi wakapigane vita kama mamluki wa Israel
(last modified Thu, 14 Nov 2024 06:53:17 GMT )
Nov 14, 2024 06:53 UTC
  • Ripoti: Ujerumani inaajiri wakimbizi wakapigane vita kama mamluki wa Israel

Mashirika ya intelijensia ya Ujerumani na ya Kizayuni kwa uratibu wa karibu na utawala wa Tel Aviv yameripotiwa kwamba, yamekuwa yakiwaajiri wakimbizi kutoka nchi zilizokumbwa na vita ili wawe mamluki wa kutumiwa vitani na Israel katika vita dhidi ya Ghaza na Lebanon.

Ripoti zinasema, katika kipindi cha miezi saba iliyopita, Jumuiya ya Mpango wa Maadili na Jumuiya ya Ujerumani na Israel (DIG) zimefanya kazi ya kusajili wakimbizi kutoka Afghanistan, Libya na Syria.
 
Wakimbizi hao wanapewa mishahara kila mwezi ya kuanzia yuro 4,000 hadi 5,000 na uraia wa Ujerumani unaofanikishwa kwa haraka. Wengi wamejiunga na kampeni ya utawala dhalimu wa Israel ya kufanya mauaji ya kimbari huko Ghaza na katika uvamizi dhidi ya Lebanon.
 
Ripoti zimeendelea kueleza kuwa, katika kipindi cha kati ya Septemba na Oktoba pekee, wakimbizi wapatao 4,000 walipewa uraia wa Ujerumani.

Ujerumani imethibitisha na kuonyesha hadharani inavyouunga mkono kwa kila hali utawala wa Kizayuni wa Israel.

 
Kufuatia Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa ya Oktoba 7, 2023, Ujerumani iliweka vizuizi zaidi kwa waombaji uraia kutoka nchi za Kiarabu na Kiislamu.
 
Lakini mapema mwezi huu, serikali ya Berlin ilianzisha sheria ya ulazima wa kujiandikisha jeshini kwa kila mwarabu na muislamu anayeomba uraia wa nchi hiyo, ikidai kwamba hatua hiyo inalenga kufidia uhaba wa nguvukazi.
 
Hata hivyo, usajili huo hauhusishi kuhudumu kijeshi nchini Ujerumani, sharti ambalo limewaacha wengi wa wakimbizi hao na wasiwasi wa wapi watapelekwa na watakwenda kupigana na nani.
 
Sera ya Ujerumani ya kuunga mkono mauaji ya kimbari huko Ghaza na ugaidi nchini Lebanon ilibainishwa wazi na waziri wa mambo ya nje Annalena Baerbock katika ziara yake ya hivi majuzi nchini Lebanon.../