Matukio ya Amsterdam dhihirisho la utambulisho halisi wa Wazayuni
(last modified Wed, 13 Nov 2024 02:15:11 GMT )
Nov 13, 2024 02:15 UTC
  • Matukio ya Amsterdam dhihirisho la utambulisho halisi wa Wazayuni

Kinyume na riwaya na simulizi iliyogeuzwa ya ghasia za Wazayuni huko Amsterdam Uholanzi, sasa Wazayuni wavamizi katika nchi nyingine za Ulaya pia wanahisi kutokuwa na usalama.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imetangaza kuwa: Tunaomba Waisraeli wikii hii wasihudhurie hafla zozote za kitamaduni na michezo nje ya Israel.

Baraza la Usalama wa Ndani la utawala wa Kizayuni pia limesema: Waisraeli wasiende Paris kutazama mechi ya timu ya soka ya Israel siku itakapomenyana na timu ya taifa ya soka ya Ufaransa Alkhamisi ya kesho. Maonyo na indhari hizi zinatolewa baada ya mashabiki wafanya fujo wa timu ya soka ya Maccabi ya Tel Aviv kuanzisha vurugu mjini Amsterdam na kukabiliwa na radiamali kali kutoka kwa wafuasi wa Palestina. Mashabiki hao ambao walikuwa wamesafiri hadi Uholanzi kutazama mchezo wa timu yao dhidi ya timu ya soka ya Ajax Amsterdam katika mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mara nyingi walisababisha vurugu na mivutano mikali walipokuwa Amsterdam.

Kufuatia dharau na matusi ya mashabiki wa Kizayuni dhidi ya bendera ya Palestina baada ya kumalizika mechi ya kandanda kati ya Ajax Amsterdam na Maccabi ya Tel Aviv, vijana wanaounga mkono Palestina walipambana vikali na Wazayuni.

Maandamano ya kuunga mkkono Palestina nchini Ireland

 

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zinaonyesha wafuasi kadhaa wa timu ya kandanda ya Israel wakichanachana bendera ya Palestina ambayo ilikuwa imetundikwa kwenye madirisha ya nyumba za mji wa Amsterdam. Kitendo hicho kiliwakasirisha sana waungaji mkono wa Palestina na kuibua mapigano kati yao. Video za mashabiki wa Kizayuni zinawaonyesha kwa pamoja wakipiga nara za kichochezi na chuki dhidi ya Waarabu na Wapalestina.

Klabu ya Maccabi ya Tel Aviv ina mashabiki wa Kizayuni waliofurutu ada zaidi katika utawala wa Kizayuni, jambo linalowafanya wafahamike kwa tabia hiyo ya kihuni na ufanyaji ghasia na fujo katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu na dunia nzima kwa ujumla.

Katika moja ya video hizo, inaonekana wazi wafuasi wafanya ghasia wa timu ya Maccabi wakipiga nara dhidi ya viongozi wa muqawama na kutoa wito wa kuuawa Wapalestina zaidi wakiashiria vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya Gaza. Pamoja na hayo, misimamo mikali ya waungaji mkono wa Palestina dhidi ya ghasia za Wazayuni wa Uholanzi imezifanya mamlaka za Kizayuni kuwa na wasiwasi wa kurudiwa matukio ya aina hiyo katika nchi nyingine za Ulaya.

Uchambuzi wa matukio ya hivi karibuni ya Amsterdam na misimamo ya kimataifa kuhusu ukatili wa Israel dhidi ya Wapalestina unaonyesha kupanuka kwa gumzo ambalo ndani yake lina uungaji mkono kwa Palestina na upinzani dhidi ya sera za Wazayuni na hali hiyo inaonekana kufikia kiwango cha kimataifa na cha juu. Mjadala huu umeakisiwa kwa kiasi kikubwa katika nyanja kama vile za kisiasa, kijamii na vyombo vya habari na ni ishara ya mabadiliko ya kimuundo katika namna ulimwengu unavyolitazama suala la Palestina na Israel.

Maandamano ya kulaani jinai za Israel 

 

Matukio ya hivi karibuni, hasa barani Ulaya, yanaonyesha kwamba, maoni ya umma yamo katika hali ya kubadilika. Huko Amsterdam na miji mingine kadhaa ya Uholanzi, watu walijitokeza kwa hiari mitaani kuwaunga mkono Wapalestina, na hata katika mashindano ya michezo na kuonyesha kuchukizwa na tabia ya Wazayuni.

Hii inaonyesha kuwa fikra za umma Ulaya zana ufahamu na welewa zaidi juu ya jinai dhidi ya Wapalestina kuliko hapo awali na inaonyesha unyeti zaidi dhidi yake.

Filihali, serikali nyingi za Ulaya na viongozii wake wamekabiliwa na mashinikizo ya maoni ya umma. Misimamo ya kisiasa inaweza kuwa haijabadilika haraka katika ngazi rasmi, lakini mikutano ya hadhara, maandamano, na hata mivutano ya mitaani inaonyesha mabadiliko katika ngazi ya umma na hatimaye inaweza kuathiri sera rasmi pia.

Mwenendo huu unaonyesha kuwa, licha ya kuwa Israel ingali inajaribu kuzuia mabadiliko makubwa kwa kutumia ushawishi wake na uhusiano wa kimataifa, lakini nguvu ya mazungumzo ya umma ya kuunga mkono Palestina na upinzani dhidi ya uvamizi wa Israel na jinai zake za kila uchao imefikia katika hatua ambayo haiwezekani tena kupuuzwa na kufumbiwa macho.