Maporomoko ya udongo yaua watu 16 magharibi ya Madagascar
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i118838-maporomoko_ya_udongo_yaua_watu_16_magharibi_ya_madagascar
Watu wapatao 16 wamefariki dunia wakati mashua waliyokuwa wakisafiria kupitia mtoni magharibi mwa Madagascar kukumbwa na maporomoko ya udongo. Hayo yameelezwa na mamlaka husika za nchi hiyo jana Jumatano.
(last modified 2025-11-10T09:13:24+00:00 )
Nov 14, 2024 07:05 UTC
  • Maporomoko ya udongo yaua watu 16 magharibi ya Madagascar

Watu wapatao 16 wamefariki dunia wakati mashua waliyokuwa wakisafiria kupitia mtoni magharibi mwa Madagascar kukumbwa na maporomoko ya udongo. Hayo yameelezwa na mamlaka husika za nchi hiyo jana Jumatano.

Kwa mujibu wa Wakala wa Safari za Baharini, Bandari na Mito wa nchini Madagasacr ajali hiyo kwenye Mto Tsiribihina ilitokea Jumanne usiku.
 
Taarifa iliyotolewa na wakala huo imesema, boti hiyo, ikiwa na abiria 26, ilisimama kwenye bandari karibu usiku wa manane, wakati maporomoko ya ardhi yalipopiga eneo hilo, na kuua watu 16 papo hapo. Abiria kumi waliokolewa wakiwa salama.
 
Imeelezwa kuwa, boti hiyo ilikuwa ikisafiri kati ya Belo sur Tsiribihina na Ankalalaobe, miji miwili iliyoko katika eneo la Menabe.../