-
Hizbullah: Mazungumzo na adui hayana maslahi na taifa
Nov 06, 2025 10:44Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesitiza kuwa kufanya mazungumzo na adui si kwa maslahi yoyote ya kitaifa, na kubainisha kuwa baadhi walijaribu kukabidhi silaha za muqawama dhidi ya adui kama ushahidi wa nia njema ya Lebanon.
-
Israel yaendelea kukiuka makubaliano na Lebanon, yashambulia na kuua watu 4 na kujeruhi 3
Nov 02, 2025 06:27Shambulio la anga lililofanywa na jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limesababisha vifo vya watu wanne na kuwajeruhi wengine watatu kusini mwa Lebanon ukiwa ni mwendelezo wa mashambulizi ya kigaidi yanayofanywa na Tel Aviv ndani ya ardhi ya nchi hiyo, ambayo yanakiuka makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa mwishoni mwa Novemba 2024 kati ya Harakati ya Muqawama ya Hizbullah na utawala huo ghasibu.
-
Naeem Qassem: Muqawama ni nembo ya nguvu ya Lebanon, unapaswa kulindwa
Nov 01, 2025 07:23Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani inadai kwamba inataka kutatua matatizo ya Lebanon lakini nchi hiyo sio mpatanishi mwadilifu asiyependelea upande wowote na ni mshirika katika uhalifu na jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran yalaani vikali shambulio la Israel kusini mwa Lebanon lililoua watu na kusababisha hasara kubwa
Oct 12, 2025 06:25Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amelaani vikali mashambulio ya kijeshi yanayofanywa kila mara na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Lebanon na kuendelea kukiuka mamlaka ya utawala na umoja wa ardhi ya nchi hiyo hususan shambulio la jana Jumamosi la ndege zisizo na rubani lililolenga kijiji cha Al-Musayleh.
-
Kumbukumbu ya miaka 43 ya mauaji ya Sabra na Shatila yaliyofanywa na Israel na kuitikisa dunia
Sep 16, 2025 12:06Mauaji ya Sabra na Shatila ni mfano mmoja tu wa jinai za kutisha zilizofanywa na utawala wa Israel huko Lebanon na kuitikisa dunia mwaka 1982, ambapo mauaji hayo leo yametimiza miaka 43.
-
UN: Israel imewadondoshea maguruneti askari wetu wa kulinda amani Lebanon
Sep 03, 2025 06:47Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Mataifa cha Kulinda Amani nchini Lebanon (UNIFIL) kimesema kuwa ndege zisizo na rubani za Israel zilidondosha maguruneti manne karibu na kambi ya walinda amani waliokuwa wakifanya kazi ya kuondoa vizuizi vya barabarani Jumanne asubuhi.
-
Israel yaua watu 12 Lebanon katika ukiukaji mkubwa zaidi wa usitishaji vita
Jul 15, 2025 17:42Jeshi la utawala wa kizayuni wa Israel limewaua shahidi watu wasiopungua 12 katika mashambulizi ya kinyama ya anga mashariki mwa Lebanon katika ukiukaji mkubwa zaidi wa usitishaji mapigano ambao ulianza kutekelezwa Novemba mwaka jana
-
Lebanon: Hatuna azma ya kuufanya wa kawaida uhusiano wetu na Israel
Jul 11, 2025 16:26Rais Joseph Aoun wa Lebanon amesema nchi hiyo haina mpango wa kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel kwa sasa.
-
Lebanon yakanusha madai ya kuwepo silaha katika ngome ya Hizbullah
Jun 09, 2025 11:12Jeshi la Lebanon linasema kuwa limekamilisha oparesheni zake za ukaguzi wa silaha na zana za kijeshi katika kitongoji cha Dahiyeh, kusini mwa Beirut, ngome ya Harakati ya Muqawama ya Hizbullah, bila kupata chochote cha kutia shaka.
-
Iran yaalani vikali mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon
Apr 02, 2025 07:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika eneo la Dhahiya katika mji mkuu wa Lebanon, Beirut.