Hizbullah: Mazungumzo na adui hayana maslahi na taifa
https://parstoday.ir/sw/news/daily_news-i132866-hizbullah_mazungumzo_na_adui_hayana_maslahi_na_taifa
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesitiza kuwa kufanya mazungumzo na adui si kwa maslahi yoyote ya kitaifa, na kubainisha kuwa baadhi walijaribu kukabidhi silaha za muqawama dhidi ya adui kama ushahidi wa nia njema ya Lebanon.
(last modified 2025-11-06T10:46:49+00:00 )
Nov 06, 2025 10:44 UTC
  • Hizbullah: Mazungumzo na adui hayana maslahi ya taifa
    Hizbullah: Mazungumzo na adui hayana maslahi ya taifa

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imesitiza kuwa kufanya mazungumzo na adui si kwa maslahi yoyote ya kitaifa, na kubainisha kuwa baadhi walijaribu kukabidhi silaha za muqawama dhidi ya adui kama ushahidi wa nia njema ya Lebanon.

Katika ujumbe wa wazi kwa viongozi mihimili mitatu ya nchi hiyo na wananchi wa Lebanon, Hizbullah imesisitiza kuwa: Matukio yamethibitisha kuwa Lebanon na Hizbullah zimeshikamana kithabiti na maudhui ya makubaliano ya usitishaji vita kuanzia dakika ya kwanza kabisa hadi hivi leo, lakini adui Mzayuni ameendeleza hujuma zake za ardhini, anga na baharini na ukiukaji wa makubaliano hayo hadi leo.

Sambamba na kuashiria uamuzi wa haraka wa serikali ya Lebanon kufungia silaha, Hizbullah imetangaza: "Baadhi walijaribu kukabidhi silaha zetu kwa adui kama ushahidi wa nia njema ya Lebanon." Ujumbe huo pia ulisema: "Adui alitumia  fursa ya makosa ya serikali kutumia suala la kupokonya silaha muqawama kote Lebanon kama sharti la kusimamisha uvamizi Lakini Walebanon wote wanapaswa kutambua kwamba adui wa Israel sio tu anailenga Hizbollah, bali Lebanon yote."