-
Israel yashambulia Lebanon, yakiuka makubaliano ya usitishaji vita
Feb 07, 2025 07:52Jeshi la Israel limefanya mashambulizi kadhaa ya anga dhidi ya maeneo tofauti ya kusini na mashariki mwa Lebanon, huo ukiwa ni ukiukaji mkubwa na wa wazi wa makubaliano ya kusitisha mapigano kati yake na nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Kiongozi Muadhamu amteua Naim Qassem kuwa mwakilishi wake Lebanon
Feb 05, 2025 12:29Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, katika dikrii, amemuarifisha Katibu Mkuu wa Harakati ya Muqawamaya ya Hizbullah, Sheikh Naim Qassem kama mwakilishi wake nchini Lebanon.
-
Mkuu wa Hizbullah: Lebanon haitasahau msaada wa Iran, Iraq wakati wa vita vya Israel
Jan 28, 2025 08:03Katibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, watu wa Lebanon hawatasahau uungaji mkono na msaada mkubwa waliopewa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Iraq wakati wa mashambulizi makali ya anga na nchi kavu ya Israel dhidi ya nchi yao.
-
Imam Khamenei apongeza ujasiri wa wananchi wa Lebanon
Jan 27, 2025 13:21Akaunti rasmi ya mtandao wa kijamii wa X ya Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei imetuma ujumbe kufuatia kitendo cha kijasiri cha wananchi wa Lebanon kusini mwa nchi hiyo ya Kiarabu.
-
UNIFIL yasisitiza kuondoka Lebanon wanajeshi wa Israel
Jan 27, 2025 07:08Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kusini mwa Lebanon (UNIFIL) kimetaka kuondoka kikamilifu wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel huko kusini mwa Lebanon.
-
"Hatutajadili mamlaka ya Lebanon", asema Rais Aoun baada ya Israel kuua Walebanon 15
Jan 27, 2025 02:25Rais wa Lebanon, Joseph Aoun amesema "mamalaka ya kujitawala Lebanon na ardhi yake ni jambo lisiloweza kujadiliwa". Amesema hayo baada ya vikosi vya Israel kuwafyatulia risasi na kuwaua Walebanon waliokuwa wamekimbia makazi yao kusini mwa Lebanon na waliokuwa wakirejea katika miji yao, huku muhula wa mwisho wa kuondoka askari hao makatili ukimalizikka.
-
Iran yakanusha tuhuma za Israel za kupeleka silaha Lebanon
Jan 25, 2025 11:35Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa amepuuzilia mbali madai ya Israel kamba Jamhuri ya Kiislamu inasafirisha kimagendo silaha kwenda Lebanon.
-
Israel haitaondoa askari wake kusini mwa Lebanon kama ilivyoafikiwa, Marekani yaiunga mkono
Jan 25, 2025 06:14Vyombo vya habari vya Kiebrania vimeripoti kuwa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel halitaondoka kusini mwa Lebanon utakapomalizika muhula uliowekwa wa siku 60 kesho Jumapili kulingana na makubaliano ya kusitisha vita yaliyofikiwa kati ya Israel na harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon ya Hizbullah.
-
Gazeti la Kiebrania la Haaretz: Israel imeidhinisha mpango wa kuondoa askari wake Ukanda wa Ghaza
Jan 13, 2025 03:26Gazeti la Kiebrania la Haaretz limeripoti kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha mipango ya kuwaondoa wanajeshi katika Ukanda wa Ghaza, baada ya hatua zilizopigwa katika mazungumzo ya kubadilishana mateka na harakati ya Hamas.
-
Pezeshkian ampongeza Rais mpya wa Lebanon; asisitiza umoja na kuimarisha utulivu
Jan 11, 2025 02:58Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amemtumia ujumbe Rais mpya wa Lebanon na kusisitiza kuwa umoja na kuimarisha utulivu vitazima njama za kujitanua na tamaa za adui Mzayuni dhidi ya Lebanon.