Maafisa watano wa jeshi la Israel waangamizwa kaskazini mwa Ghaza
Maafisa wengine watano wa jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel wameangamizwa na wanamapambano wa Kiislamu kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza katika kipindi cha saa 24 zilizopita.
Vyombo vya mbalimbali vya habari vimeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, baada ya kuangamizwa wanajeshi wengine wanne kaskazini mwa Ukanda wa Ghaza katika mapigano na wanamapambano wa Kiislamu, kumeifanya idadi ya wanajeshi wa Israel waliongamizwa katika kipindi cha saa 24 zilizopita kufikia wanajeshi watano akiwemo afisa mmoja wa ngazi za juu wa jeshi katili la Israel.
Kwa upande wake shirika la habari la Tasnim limenukuu vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vikitangaza habari hiyo na kusema kuwa idadi ya wanajeshi wa Israel waliongamizwa kaskazini mwa Ghaza imeongezeka kwenye kipindi cha saa 24 zilizopita akiwemo afisa mmoja wa ngazi za juu wa jeshi la utawala wa Kizayuni.
Vyombo hivyo vya habari vya Kizayuni vimetangaza kuwa, wanajeshi wanne wa Israel walioangamizwa ni kutoka Brigedi ya Kfir na vimetaja majina ya wanajeshi hao wa utawala wa Kizayuni walioangamizwa, mmoja baada ya mwingine.
Gazeti la Kizayuni la Yedioth Ahronoth limetaja majina ya maafisa wanne wa jeshi la Israel walioangamizwa kaskazini mwa Ghaza kuwa ni: Sajenti Orr Katz, 20, kutoka Ma’ale Adumim, Sajenti Nave Yair Asulin, 21, kutoka Carmit, Sajenti Gary Lalhruaikima Zolat, 21, kutoka Afula na Sajenti Ofir Eliyahu, 20 kutoka Holon.
Kabla ya hapo jeshi la utawala wa Kizayuni lilikuwa limetangaza habari ya kuangamizwa afisa wake mwingine wa ngazi za juu kutoka kikosi cha Lotar, kaskazini mwa Ghaza.