Wananchi wa Morocco waandamana kuunga mkono Palestina
(last modified Sat, 16 Nov 2024 12:24:09 GMT )
Nov 16, 2024 12:24 UTC
  • Wananchi wa Morocco waandamana kuunga mkono Palestina

Wananchi wa Morocco wameandamana na kutangaza himaya na uungaji mkono wao kwa wananchi wa Gaza na kulaani jinai za utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Washiriki wa maandamano hayo wamesisitiza kuendelea kwa maandamano yao ya amani hadi pale vita vitakapokoma na Wapalestina kufurahia haki zao za haki, ikiwa ni pamoja na kuundwa taifa huru la Palestina.

Waandamanaji walitoa nara za kuunga mkono muqawama wa Wapalestina na kupinga vita na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Gaza, Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Palestina yote, pamoja na uungaji mkono wa Marekani na Magharibi kwa Israel na "kimya" cha ulimwengu wa Kiarabu.

Kadhalika waandamanaji hao wametoa mwito wa kupelekwa haraka misaada ya kibinadamu huko Gaza na Lebanon sambamba na kuchukuliwa hatua za kusitishwa mauaji na jinai zinazofanywa na utawala ghasibu wa Israel.

Katika majuma ya hivi karibuni, mataifa mbalimbali ya Kiafrika yakiwemo ya Morocco, Mauritania, Tunisia, Algeria na Nigeria yamekuwa yakishuhudia maandamano mara kwa mara ya kuwaunga mkono Wapalestina na Walebanon na wakati huo huo kulaani jinai na mauaji ya kimbari yanayofanywa na Israel kwa uungaji mkono kamili wa Marekani na washirika wake.