-
Baraza la Uongozi la Sudan lasisitiza kuwa liko tayari kushirikiana na UN
Dec 01, 2025 06:55Mkuu wa Baraza Kuu la Mpito la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan, amesema kuwa serikali yake iko tayari kushirikiana na Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono juhudi za kibinadamu, maendeleo na jitihada za kijamii za nchi hiyo.
-
Wabeba silaha wateka nyara watu wengine 14 Nigeria, yumo bibi harusi na kitoto kichanga
Dec 01, 2025 02:14Washambuliaji wenye silaha wamewateka nyara wanawake 13 na mtoto mchanga katika hujuma mpya ya uvamizi uliofanywa usiku wa kuamkia jana Jumapili kaskazini mashariki mwa Nigeria, ukiwa ni mwendelezo wa matukio ya hivi karibuni ya utekaji nyara mkubwa unaoshuhudiwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi.
-
Rais wa Afrika Kusini amtuhumu Trump kwa kutoa 'kauli zisizo za kweli' kuhusu nchi yake
Nov 30, 2025 23:37Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alimtuhumu Rais Donald Trump wa Marekani kwa kuendelea kutoa "taarifa zisizo za kweli" kuhusu nchi yake.
-
Ushahidi wa kwanza: Gesi ya klorini imetumika katika vita vya ndani Sudan
Nov 30, 2025 08:57Uchunguzi wa timu ya FRANCE 24 Observers unaonyesha namna gesi ya klorini ilivyotumika kama silaha katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea nchini Sudan.
-
Marais wa Rwanda na DRC kutia saini makubaliano ya amani
Nov 30, 2025 04:11Marais Felix Tshisekedi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame wiki ijayo wanatarajiwa kutia kusaini makubaliano ya mwisho yanayolenga kufikia amani ya kudumu mashariki mwa Congo.
-
Spika wa bunge la Libya atoa mwito wa kufanyika uchaguzi wa haraka wa rais
Nov 29, 2025 23:06Spika wa Bunge la Libya lenye makao yake mashariki mwa nchi hiyo ametoa mwito kwa Tume Kuu ya Uchaguzi kutekeleza mara moja sheria ya kuitisha haraka uchaguzi wa rais wa moja kwa moja.
-
Bunge la Ulaya lakosolewa kwa kuingilia mambo ya Tanzania
Nov 29, 2025 04:02Ulaya imekosolewa kwa “kujipa haki ya kujadili kila kinachotokea Afrika,” mfano wa karibuni ukiwa ukosoaji wa Bunge la Ulaya kuhusu uchaguzi nchini Tanzania.
-
Mapigano yaibuka mashariki mwa DRC, wakimbizi waongezeka
Nov 29, 2025 03:56Mapigano mapya kati ya waasi wa M23 na jeshi la amhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, likisaidiwa na wanamgambo wanaojulikana kamma Wazalendo, yamesababisha wakazi wengi kuyahama makazi yao katika maeneo kadhaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Umoja wa Afrika wasimamisha uanachama wa Guinea-Bissau kufuatia mapinduzi ya kijeshi
Nov 29, 2025 03:52Umoja wa Afrika (AU) umetangaza kuizuia mara moja Guinea-Bissau kushiriki katika shughuli zake zote hadi utaratibu wa kikatiba utakaporejeshwa nchini.
-
Adolf Hitler ashinda kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa Namibia
Nov 28, 2025 23:56Mwanasiasa wa Namibia aliyepewa jina la dikteta wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler, ametangazwa mshindi kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa, kwa mujibu wa matokeo rasmi yaliyoripotiwa Ijumaa.