-
Rais wa Guinea-Bissau akimbilia Senegal baada ya mapinduzi ya kijeshi
Nov 28, 2025 23:53Rais wa Guinea-Bissau aliyeondolewa madarakani, Umaro Sissoco Embaló, amekimbilia nchi jirani ya Senegal baada ya jeshi kuchukua mamlaka kufuatia uchaguzi ulioibua utata, maafisa wamesema.
-
Kagame: Nina matumaini mazungumzo yangu na Tshisekedi yatakuwa chanya
Nov 28, 2025 08:13Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema ana matumaini kuwa, mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Marekani kati yake na Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yataleta matokeo chanya.
-
Afrika Kusini yailaani Marekani kwa kuizuia kushiriki Mkutano wa G20 wa 2026
Nov 28, 2025 03:03Afrika Kusini imelaani nia ya rais wa Marekani Donald Trump ya kuizuia nchi hiyo kuhudhuria Mkutano wa Kundi la 20 (G20) huko Miami, Florida, mwaka ujao.
-
Oxfam: Nusu ya Wakenya katika umasikini; matajiri 125 wanamiliki utajiri wa watu milioni 42.6
Nov 27, 2025 23:30Ripoti iliyotolewa na Shirika la Oxfam inaonyesha kuwa, matajiri 125 wanamiliki zaidi ya utajiri wa Wakenya milioni 42.6, huku nusu ya wananchi wakiishi kwa chini ya KSh130 kwa siku.
-
Kwa nini Afrika inataka kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Nov 27, 2025 23:27Bara la Afrika, kwa miaka kadhaa sasa, limekuwa likitafuta kiti cha kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
-
Wanajeshi Guinea-Bissau wamtangaza Jenerali Horta Inta-A kuwa kiongozi wa kijeshi wa nchi hiyo
Nov 27, 2025 11:10Askari waliofanya mapinduzi ya kijeshii nchini Guinea-Bissau leo Alkhamisi wametangaza kiongozi mpya wa kijeshi wa nchi hiyo, wakiimarisha unyakuzi wa madaraka ulioanza baada ya uchaguzi wa rais nchini humo.
-
Rais wa Nigeria atangaza hali ya hatari kufuatia wimbi la utekaji nyara
Nov 27, 2025 08:55Rais wa Nigeria, Bola Tinubu, ametangaza hali ya hatari ya kiusalama nchini humo baada ya mauaji na utekaji nyara kuongezeka kwa kasi.
-
Waangalizi wa uchaguzi walaani mapinduzi ya kijeshi Guinea-Bissau
Nov 27, 2025 08:53Viongozi wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika (AU), Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) pamoja na Jukwaa la Wazee wa Afrika Magharibi (WAEF) wameeleza “wasiwasi mkubwa” kufuatia mapinduzi ya kijeshi yaliyotokea Guinea-Bissau baada ya uchaguzi wa urais.
-
Wakimbizi 115 wa Burundi warudishwa nyumbani kutokea Rwanda
Nov 27, 2025 02:29Wakimbizi 115 wa Burundi, ambao wengi wao walikuwa wamekimbilia Rwanda mwaka huu wa 2015 kutokana na machafuko ya kisiasa nchini mwao, wamerudishwa kwa hiari nchini Burundi. Hayo ni kwa mujibu wa Wizara ya Usimamiaji wa Masuala ya Dharura ya Rwanda.
-
Tunisia yamwita Balozi wa EU ili ajieleze kwa kukiuka itifaki ya kidiplomasia
Nov 27, 2025 02:28Rais Kais Saied wa Tunisia amemwita Giuseppe Perrone, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini humo na kumtaka ajieleze kwa kufanya uchochezi na kutoheshimu itifaki za kidiplomasia. Hayo yametangazwa na Ikulu ya Rais mjini Tunis.