-
Umoja wa Afrika wakaribisha kutiwa saini kwa mkataba wa amani kati ya DRC na waasi
Nov 17, 2025 05:39Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Mahmoud Ali Youssouf, amepongeza kutiwa saini kwa makubaliano ya amanikati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na waasi hayo akisema ni “hatua kubwa kuelekea kurejesha uthabiti, kujenga tena imani, na kushughulikia mizizi ya migogoro mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).”
-
Vyombo vya usalama Tanzania vyamkamata raia wa Marekani na Kenya akiwa na mabomu
Nov 17, 2025 00:16Polisi ya Tanzania imetangaza kuwa imemkamata raia wa Marekani na Kenya akiwa na mabomu katika mpaka wa Tanzania na Kenya.
-
Somalia yakaribia uchaguzi wa moja kwa moja, wakazi wa Mogadishu wachukua kadi za kupiga kura
Nov 16, 2025 23:17Somalia imezindua rasmi ugawaji wa kadi za wapiga kura katika mji mkuu, Mogadishu, kuelekea uchaguzi wa manispaa, hatua muhimu katika safari ya taifa hilo kuelekea uchaguzi wa ushiriki wa moja kwa moja wa upigaji kura.
-
Israel yamuua kigaidi mtaalamu mwingine wa nyuklia wa Misri
Nov 16, 2025 07:28Ingawa maafisa wa Misri wametangaza kwamba wamemkamata mhusika wa mauaji ya mwanasayansi kijana wa nyuklia wa nchi hiyo; lakini taarifa nyingine zinasisitiza kwamba muuaji aliondoka eneo la tukio mbele ya macho ya kila mtu na inaaminika ana uhusiano na shirika la kijasusi la Israel MOSSAD hasa kwa kuzingatia kuwa, Tel Aviv ina historia chafu ya kufanya jinai kama hizo za kuwaua kigaidi wanasayansi wa nyuklia wa nchi mbalimbali ikiwemo Misri.
-
Watu wasiopungua 20 wauawa katika shambulio la waasi wa ADF mashariki mwa DRC
Nov 16, 2025 07:28Kwa uchache watu 20 wamepoteza maisha katika kipindi cha siku mbili za Ijumaa na Jumamosi katika shambulio lililohusishwa na waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
-
Watu 4 wapoteza maisha baada ya boti za wahamiaji kuzama kwenye pwani ya Libya
Nov 16, 2025 07:27Shiriika la Hilali Nyekundu limetangaza kuwa, kwa uchache watu wanne wamepoteza maisha wakati boti mbili zilizokuwa zimebeba wahamiaji 95 zilipozama kwenye pwani ya mji wa Al Khums wa magharibi mwa Libya.
-
Charlotte Slente: Zaidi ya nusu ya Wasudan wanahitaji msaada wa kibinadamu
Nov 16, 2025 03:37Zaidi ya nusu ya idadi ya watu wa Sudan wanahitaji msaada wa kibinadamu. Hayo yameelezwa na Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Denmark, huku mapigano yakiliharibu taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika.
-
DRC na M23 zasaini "muundo kamili" wa mpango wa amani baada ya mazungumzo ya Doha
Nov 15, 2025 22:58Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kundi la waasi la M23 zimesaini makubaliano ya muundo kwa ajili ya mkataba wa amani unaolenga kumaliza mapigano mashariki mwa nchi hiyo.
-
Afrika Kusini inafuatilia kesi ya mauaji ya kimbari yaliyofanywa na Israel
Nov 15, 2025 08:00Serikali ya Afrika Kusini imetangaza kuwa, itaendelea kuchukua hatua za kisheria dhidi ya Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa tuhuma za kutenda mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Ramaphosa: Hatutowarudisha Wapalestina waliokuja Afrika Kusini
Nov 15, 2025 01:52Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, makumi ya Wapalestina waliofika nchini humo kwa ndege ya kukodi hawatarudishwa bali watapewa hifadhi nchini Afrika Kusini.