-
Rais wa Tanzania atoa msamaha kwa vijana waliofanya fujo wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu
Nov 15, 2025 01:51Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa vijana waliofanya fujo wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 akisema kuwa, walifuata mkumbo na hawakujua walifanyalo.
-
Mashambulizi ya anga yaendelea Libya, 71 waokolewa baharini
Nov 15, 2025 01:51Mji wa Zawiya wa magharibi mwa Libya ulioko umbali wa kilomita 60 magharibi mwa mji mkuu Tripoli, umekumbwa na mashambulizi ya mfululizo ya anga. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya karibuni kabisa ya Shirika la Kudhibiti Vitisho vya Usalama mjini Zawiya.
-
Jenerali Al Burhan hakutakuwa na suluhu baina ya SAF na RSF
Nov 15, 2025 01:50Mkuu wa jeshi la Sudan SAF Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan alisema jana Ijumaa kwamba hakutakuwa na "suluhu wala amani" kati ya jeshi analoongoza yeye SAF na Vikosi vya Msaada wa Haraka RSF akisisitiza kwamba operesheni za kijeshi zitaendelea hadi "watakaposambaratishwa kabisa wanamgambo waasi."
-
Samia amwapisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania
Nov 14, 2025 07:42Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amemwapisha Dk. Mwigulu Lameck Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya kuthibitishwa na Bunge jana Alkhamisi Novemba 13, 2025.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Congo DR: Rwanda lazima ionyeshe hamu ya kweli ya kutaka amani
Nov 14, 2025 06:44Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Thérèse Kayikwamba Wagner, ameikosoa vikali Rwanda, akiitaka ithibitishe dhamira yake ya kweli ya kutaka amani, kutokana na uwepo wa vikosi vyake ndani ya ardhi ya Congo na mvutano unaoongezeka mashariki mwa nchi hiyo.
-
CDC: Afrika inakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika miaka 25
Nov 14, 2025 06:09Shirika la Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa Afrika (CDC) limetahadharisha kuwa bara la Afrika linakabiliwa na mlipuko mbaya zaidi wa kipindupindu katika kipindi cha robo karne, likifungamanisha ongezeko hilo na miundombinu dhaifu ya maji na migogoro inayoendelea katika sehemu mbalimbali za bara hilo.
-
Baraza la Haki za Binadamu la UN linapigia kura rasimu ya azimio kuhusu Sudan
Nov 14, 2025 05:41Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa leo Ijumaa, litapiga kura katika kikao maalumu kinachojadili mgogoro wa Sudan, kuhusu rasimu ya azimio linalolaani ukiukwaji wa haki za binadamu ambao linasema umefanywa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) ndani na karibu na mji wa El Fasher katika shambulio la hivi karibuni la wapiganaji wa kundi hilo dhidi ya mjini huo.
-
Kwa nini kutoshiriki Marekani katika kikao cha G20 nchini Afrika Kusini ni hasara kubwa kwa Washington?
Nov 14, 2025 04:39Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa kutohudhuria Wamarekani katika kikao cha G20 ni hasara kubwa kwao.
-
UN yamchagua Profesa Phoebe Okowa wa Kenya kuwa Jaji wa Mahakama ya ICJ
Nov 14, 2025 04:12Katika kura ya kihistoria iliyopigwa Umoja wa Mataifa siku ya Alkhamisi, profesa wa sheria wa Kenya Phoebe Okowa alichaguliwa kuwa jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ), akiibuka mshindi kwenye ulingo wa ushindani wa wagombea wa Kiafrika baada ya mfululizo wa raundi za kupiga kura zilizokuwa na mvutano katika Baraza Kuu na Baraza la Usalama.
-
Bunge la Tanzania lamthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo
Nov 13, 2025 10:20Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo Alhamisi limemthibitisha Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo baada ya kupata kura 369 kati ya kura 371 zilizopigwa na wabunge. Baada ya uthibitisho huo, Dkt. Nchemba ataapishwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kuanza mara moja majukumu yake.