-
Mudavadi: Zaidi ya Wakenya 200 wanapigana pamoja na Russia katika vita vya Ukraine
Nov 13, 2025 10:19Serikali ya Kenya imesema kwamba zaidi ya raia wake 200 wanapigana katika safu ya jeshi la Russia katika vita vyake dhidi ya Ukraine, ikionya kwamba mitandao ya kuajiri wapiganaji bado inaendelea kufanya kazi na inawalenga Wakenya kwa kutoa kazi zenye kipato kikubwa.
-
Ni ipi nafasi ya pande za kigeni katika mgogoro wa Sudan?
Nov 13, 2025 09:25Vita nchini Sudan vimechukua sura mpya kufuatia kuendelea uingiliaji kati wa nchi ajinabi nchini humo na kudhibitiwa mji wa Al Fasher na wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF).
-
Katibu Mkuu wa UN: Dunia isiliache mkono bara la Afrika, lina uwezo mkubwa mno
Nov 13, 2025 09:05Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, amesema dunia haiwezi kulipa kisogo bara la Afrika akisisitiza kuwa bara hilo ni nyumbani kwa karibu robo ya watu wote duniani, na lina nafasi kubwa ya maendeleo.
-
Mali yakanusha hofu kwamba magaidi wanakaribia kuudhibiti mji mkuu, Bamako
Nov 13, 2025 09:04Waziri wa Mambo ya Nje wa Mali amepuuzilia mbali dhana kwamba magaidi hivi karibuni wanaweza kuudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo, Bamako. Hii ni radiamali ya kwanza kutolewa na serikali kuhusu wasiwasi na hofu ya usalama katika nchi ya Mali ambayo imechochea nchi za Magharibi kuwataka raia wao waondoke nchini humo.
-
Kamisheni ya Umoja wa Afrika yakanusha madai ya Trump kuhusu mauaji ya Wakristo Nigeria
Nov 13, 2025 03:50Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) amekanusha vikali madai ya Rais wa Marekani, Donald Trump, kuhusu mauaji ya kimbari dhidi ya Wakristo kaskazini mwa Nigeria.
-
Rais wa Afrika Kusini: Kutohudhuria Marekani mkutano wa G20 ni hasara kwake
Nov 13, 2025 03:48Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa, kitisho cha Rais wa Marekani Donald Trump kwamba maafisa wa nchi yake hawatahudhuria mkutano wa G20 mjini Johannesburg ni hasara kwa Wamarekani.
-
Dkt. Mwigulu Nchemba ateuliwa Waziri Mkuu mpya wa Tanzania
Nov 13, 2025 02:52Rais Samia Suluhu Hassan leo amewasilisha bungeni jina la Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu mpya wa serikali ya awamu ya sita ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
-
Umoja wa Mataifa wataka uchunguzi kwa mauaji Tanzania
Nov 12, 2025 23:06Umoja wa Mataifa umetowa wito wa kufanyika uchunguzi kwa kile kinachodaiwa kuwa vifo vya mamia ya watu katika machafuko ya kupinga uchaguzi nchini Tanzania.
-
Museveni aonya: Vita vitatokea Afrika ikiwa nchi zisizo na bandari zitashindwa kufikia Bahari ya Hindi
Nov 12, 2025 08:08Katika kauli iliyotafsiriwa kama onyo lililolenga nchi jirani, Rais Yoweri Museveni wa Uganda ameonya kuhusu uwezekano wa kutokea vita katika siku zijazo endapo nchi za Afrika ambazo hazina bandari zitaendelea kunyimwa haki ya kufikia Bahari ya Hindi.
-
Shirika la Umoja wa Mataifa: Kuna Ushahidi wa matumizi ya kimfumo ya ubakaji nchini Sudan
Nov 12, 2025 04:09Shirika la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Wanawake limeonya kwamba kuna "ushahidi unaoongezeka kwamba ubakaji unatumika kwa makusudi na kwa utaratibu maalumu" nchini Sudan, huku njaa na ukosefu wa usalama wa chakula vikiendelea kutesa watu nchini humo.