-
Rais wa Iran afanya mazungumzo na Amir wa Qatar
Sep 15, 2025 07:50Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo amekutana na kufanya mazungumzo na Amir wa Qatar katika mji mkuu wa nchi hiyo Doha.
-
Araghchi: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko bega kwa bega na Qatar na Waislamu wote
Sep 15, 2025 02:55Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye yuko mjini Doha, Qatar kushiriki katika mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Kiislamu na Kiarabu, amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu iko bega kwa bega na ndugu zake Waislamu wote.
-
Iran yapinga madai ya G7, na kuyataja kuwa ya uongo
Sep 14, 2025 05:38Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha vikali tuhuma zilizotolewa katika taarifa ya pamoja ya G7 na washirika wake, ikizitaja kuwa ni za kupotosha, zisizo na msingi, na ni mbinu ya kisiasa ya kujiepusha na lawama.
-
Juhudi za mhimili wa Magharibi za kuchafua jina la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Sep 14, 2025 04:46Wanachama wa Mchakato wa Radiamali ya Haraka wa Kundi la G7 ambazo ni nchi za Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan, Uingereza, Marekani na Umoja wa Ulaya, pamoja na Australia na New Zealand, katika taarifa ya pamoja siku ya Ijumaa walidai kulaani hatua za Iran kuhusiana na eti kuongezeka kwa kampeni ya ukandamizaji unaotekelezwa nje ya mipaka yake.
-
Iran yazionya Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani kuhusu vikwazo
Sep 14, 2025 03:29Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, ametoa onyo kali kwa Uingereza, Ufaransa, na Ujerumani kwamba iwapo zitaendeleza juhudi zao za kuanzisha tena vikwazo vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran, basi zitakumbwa na madhara yasiyoweza kurekebishwa.
-
Mkuu wa zamani IRGC azitahadharisha Saudia, Uturuki na Iraq, asema; mabomu ya Israel yanawasubiri
Sep 13, 2025 23:56Kamanda Mkuu wa zamani wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amezitahadharisha nchi za eneo zikiwemo Saudi Arabia, Uturuki na Iraq kwamba ziko katika hatari ya kukabiliwa na uvamizi wa Israel iwapo nchi za kanda hii zitashindwa kuunda "muungano wa kijeshi" dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Araghchi: Iran ina azma ya kuimarisha uhusiano imara na ulimwengu wa Kiislamu
Sep 13, 2025 08:36Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amesema kuwa mahusiano kati ya Iran na Tunisia ni “mfano angavu” wa dhamira ya Tehran kuendeleza uhusiano imara na mataifa ya Kiislamu kwa msingi wa “maslahi ya pamoja na heshima kwa mamlaka ya kitaifa.”
-
Larijani azitaka serikali za Kiislamu kuchukua hatua dhidi ya jinai za Israel
Sep 13, 2025 08:02Ali Larijani, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran katika ujumbe wake amezitaka serikali za Kiislamu kuchukua hatua madhubuti na za kivitendo dhidi ya jinai za Israel.
-
Velayati: Shambulizi la Qatar laonesha kuwa Israel ‘haina mipaka’ katika uhalifu wake
Sep 12, 2025 22:59Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amesema kuwa dunia haiwezi kuendelea kufumbia macho ukatili wa Israel kufuatia mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Qatar, akieleza kuwa utawala huo haramu “hautambui mipaka” katika uhalifu wake.
-
Rais wa Iran kuhudhuria kikao cha nchi za Kiislamu na Kiarabu cha Doha kujadili uchokozi wa Israel
Sep 12, 2025 07:32Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atahudhuria kikao cha dharura cha nchi za Kiislamu na Kiarabu kitakachofanyika mjini Doha siku ya Jumapili na Jumatatu kwa wito wa serikali ya Qatar, ili kuwaunga mkono Wapalestina wa Ghaza na kuchukua hatua dhidi ya shambulio la hivi karibuni lililofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika mji mkuu wa Qatar, Doha.