Andrei Kartapolov: Russia inapinga uingiliaji wa nchi ajinabi; iko pamoja na Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i135420-andrei_kartapolov_russia_inapinga_uingiliaji_wa_nchi_ajinabi_iko_pamoja_na_iran
Mbunge wa ngazi ya juu katika bunge la Russia ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya Ulinzi katika Duma amekariri uungaji mkono wa nci yake kwa Iran na kusema Moscow inapinga uingiliaji wa nchi ajinabi khususan uingiliaji wa nchi za Magharibi katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-01-13T03:42:56+00:00 )
Jan 13, 2026 03:42 UTC
  • Andrei Kartapolov
    Andrei Kartapolov

Mbunge wa ngazi ya juu katika bunge la Russia ambaye pia ni Mkuu wa Kamati ya Ulinzi katika Duma amekariri uungaji mkono wa nci yake kwa Iran na kusema Moscow inapinga uingiliaji wa nchi ajinabi khususan uingiliaji wa nchi za Magharibi katika masuala ya ndani ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

 "Tupo pamoja na tumesimama kidete upande wa Iran,” Andrei Kartapolov aliwaambia waandishi wa habari jana Jumatatu akijibu swali  aliloulizwa kuhusu machafuko ya hivi karibuni katikamijimbalimbali ya Iran. 

Mkuu wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Russia amesema nchi hiyo ina msimamo wa wazi kuhusu haki za mataifa yote na imekuwa ikitetea haki hizo mara kwa mara.

Andrei Kartapolov amekosoa vikali njama za Marekani na Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema jitihada zozote za aina hiyo kwa lengo la kubadili mfumo wa kisasa wa Iran hazikubaliki na ni kinyume cha sheria.  

" Ni  wananchi pekee ndio wenye haki ya kubadilisha mfumo uongozi wa nchi,” ameongeza Kartapolov.

Kartapolov pia amesisitiza uungaji mkono wa Russia kwa haki ya Iran ya kustawisha nishati ya nyuklia kwa malengo ya amani na maendeleo ya jumla ya wananchi wa Iran.

Mkuu wa Kamati ya Ulinzi katika Bunge la Russia ameashiria vita vya kichokozi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kusema Warussia wako upande wa wananchi wa Iran ambao awali walishambuliwa na Israel na kisha Marekani.