-
Velayati: Shambulizi la Qatar laonesha kuwa Israel ‘haina mipaka’ katika uhalifu wake
Sep 12, 2025 22:59Mshauri mwandamizi wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei, amesema kuwa dunia haiwezi kuendelea kufumbia macho ukatili wa Israel kufuatia mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Qatar, akieleza kuwa utawala huo haramu “hautambui mipaka” katika uhalifu wake.
-
Rais wa Iran kuhudhuria kikao cha nchi za Kiislamu na Kiarabu cha Doha kujadili uchokozi wa Israel
Sep 12, 2025 07:32Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran atahudhuria kikao cha dharura cha nchi za Kiislamu na Kiarabu kitakachofanyika mjini Doha siku ya Jumapili na Jumatatu kwa wito wa serikali ya Qatar, ili kuwaunga mkono Wapalestina wa Ghaza na kuchukua hatua dhidi ya shambulio la hivi karibuni lililofanywa na utawala wa kizayuni wa Israel katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
-
Araghchi aikosoa Ulaya kwa kufumbia macho uchokozi wa US, Israel dhidi ya Iran
Sep 12, 2025 03:41Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi ameyajia juu mataifa matatu ya Ulaya kwa mtazamo wao wa "kutowajibika" mkabala wa uchokozi wa hivi karibuni wa Marekani na Israel dhidi ya Iran, pamoja na vitisho vyao vya kuhuisha maazimio yaliyobatilishwa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, jambo ambalo anaamini litazidisha tu mivutano iliyopo.
-
Kamanda Mousavi: Wananchi, wanajeshi wa Iran watasimama na Qatar
Sep 12, 2025 00:18Mkuu wa Kamandi ya Majeshi ya Iran amesema kuwa serikali, taifa na vikosi vya kijeshi vya Qatar vinapaswa kujua kwamba, Jamhuri ya Kiislamu na jeshi lake litaendelea kusimama upande wao hadi mwisho.
-
Marais wa Iran na Misri wahimiza umoja dhidi ya uvamizi wa Israel
Sep 11, 2025 03:53Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Doha yanadhihirisha kutozingatiwa kanuni na mifumo ya kimataifa.
-
Araqchi: IAEA ‘imeridhishwa kikamilifu’ na makubaliano ya ushirikiano
Sep 11, 2025 03:51Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia (IAEA) umeridhishwa kikamilifu na vipengee vya makubaliano yaliyofikiwa karibuni kati ya wakala huo na Jamhuri ya Kiislamu.
-
Qalibaf: Njia ya kukabiliana na Israel ni kupitia hatua zilizoratibiwa na za umoja wa ulimwengu wa Kiislamu
Sep 10, 2025 23:47Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameandika katika ujumbe wake kufuatia mashambulizi ya anga ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Qatar: "Njia ya kukabiliana vilivyo na mienendo ya utawala wa Kizayuni ni kupitia hatua zilizoratibiwa na za umoja wa ulimwengu wa Kiislamu."
-
Iran yakemea mashambulizi ya Israeli dhidi ya vongozi wa Hamas jijini Doha
Sep 10, 2025 07:28Iran imelaani vikali mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Israel dhidi ya viongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Ukombozi wa Palestina, Hamas, wakati walipokuwa wakijadili pendekezo la Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kusitisha mapigano huko Gaza,ikiyataja kuwa ni ukiukaji wa misingi yote ya sheria za kimataifa.
-
Wanasayansi kutoka India, Uturuki na Iran watunukiwa Tuzo ya Mustafa (SAW) ya Mwaka 2025
Sep 10, 2025 07:27Wanasayansi watatu mashuhuri ambao ni Mohammad K. Nazeeruddin kutoka India, Mehmet Toner kutoka Uturuki, na Vahab Mirrokni kutoka Iran wametangazwa kuwa washindi wa Tuzo ya Mustafa (SAW) ya mwaka 2025.
-
Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) na Imam Ja'far al-Sadiq (AS) jijini Tehran
Sep 10, 2025 07:21Asubuhi ya leo, hafla ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Mtume Mtukufu Muhammad Mustafa (SAW) na Imam Ja'far al-Sadiq (AS) imefanyika jijini Tehran katika ukumbi wa Imam Khomeini (MA), kwa ushiriki wa familia za mashahidi, wananchi wa tabaka mbalimbali, na wageni wa Mkutano wa Kimataifa wa Umoja wa Kiislamu.