Qalibaf: Mataifa ya Kiislamu ‘yanapaswa kutumia nguvu’ dhidi ya Israel
-
Spika Qalibaf akiwa ziarani huko Islamabad, ambapo jjuzi Alhamisi alikutana na kuzungumza na wasomi na wanasiasa katika ubalozi wa Iran.
Mohammad Bagher Qalibaf Spika wa Majlisi ya ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa nchi za Kiislamu "zinapasa kutumia nguvu" dhidi ya utawala wa Israel na kuonya kuwa diplomasia pekee haitazuia vitendo vya uchokozi vya Israel.
Qalibaf amebainisha haya akiwa ziarani huko Islamabad, ambapo jjuzi Alhamisi alikutana na kuzungumza na wasomi na wanasiasa katika ubalozi wa Iran.
Qalibaf alianza hotuba yake kwa kusifu uungaji mkono wa wananchi wa Pakistani kwa Iran wakati wa uvamizi wa siku 12 wa Marekani na Israel dhidi ya Iran mwezi Juni mwaka huu. Amesema, ujumbe wa Pakistan wa mshikamano wakati wa vita vya siku 12 dhidi ya Iran ulimshawishi kuifanya Pakistan kuwa kituo chake cha nje ya nchi kufanya ziara baada ya vita.
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran amesema mataifa ya Kiislamu yanapasa kutumia nguvu dhidi a utawala wa Kizayuni; Nguvu zetu ni mantiki yetu, lakini iwapo hakuna maelewano unapasa kuonyesha nguvu. Utawala wa Israel hauelewi lugha nyingine yoyote.
Mnamo Juni 13 mwakahuu Israel ilianzisha mashambulizi yasiyo na msingi dhidi ya Iran, na kusababisha vita vya siku 12 vilivyoua shahidi takriban watu 1,064 hapa nchini wakiwemo makamanda wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia na raia wa kawaida.
Marekani pia iliingia vitani kwa kushambulia kwa mabomu vituo vitatu vya nyuklia vya Iran katika ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa.