Iran iko tayari kwa mchakato wa kuzalisha ndege za abiria ilizojibunia yenyewe
Mkuu wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran amesema kuwa, baada ya kubuni na kutengeneza ndege ya mizigo, sasa wataalamu wa Iran wako katika mchakato wa kubuni na kuzalisha kwa wingi ndege za abiria.
Hossein Pourfarzaneh amesema hayo na kuongeza kuwa mchakato wa kubuni na kutengeneza ndege ya taifa ya "Simorgh" ni moja ya mihimili mikuu ya Mpango wa Saba wa Maendeleo ya Viwanda ya Iran.
Ameongeza kuwa, katika uwanja wa usafiri wa anga, nguzo zote nne kuu za tasnia hii lazima zipewe kipaumbele nazo ni mfumo wenyewe wa usafiri, viwanja vya ndege, viwanda vya usaidizi na nguvukazi. Amesema: sekta ya kubuni na kutengeneza ndege za ndani ya nchi nayo ni sehemu muhimu katika tasnia hiyo.
Mkuu wa Shirika la Usafiri wa Anga la Iran pia amesema: ndege ya "Simorgh" imepasi katika hatua za majaribio ya kiwandani na hivi karibuni imepewa kibali cha kuruka. Katika majaribio ya kuruka. Baada ya kukamilisha hatua hii, ndege hiyo itaingia katika awamu ya kupata Cheti cha Ubora na Aina ya Ndege yenyewe na kisha itafuatia hatua ya uzalishaji wa kibiashara.
Pourfarzaneh amesema: Katika mradi huu unaendeshwa kwa mkataba maalumu uliosainiwa na Shirika la Usafiri wa Anga kama msimamizi mkuu, kampuni ya utengenezaji ndege na shirika la ndege linalofanya kazi na taasisi zinazosaidia hatua zote za usanifu, uzalishaji na uendeshaji.