Watu 145 washtakiwa kwa uhaini wakidaiwa kuhusika katika maandamano ya vurugu Tanzania
-
Ghasia Tanzania
Waendesha mashtaka nchini Tanzania jana Ijumaa wamewashtaki takriban watu 145 kwa kosa la uhaini madai ya kuhusika katika maandamano ya vurugu yaliyozuka wakati wa uchaguzi wa rais na bunge wiki iliyopita.kulingana na faili za mahakama zilizoonekana na Reuters.
Mashtaka hayo ni ya kwanza dhidi ya watu wanaotuhumiwa kushiriki maandamano hayo katika siku ya uchaguzi tarehe 29 Oktoba na siku zilizofuata.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imeeleza kuwa washtakiwa "walipanga nia ya kukwamisha uchaguzi mkuu wa 2025 kwa madhumuni ya kutishia Uongozi wa nchi " na kusababisha uharibifu wa mali za serikali.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam haiwakufafanua juu ya tuhuma maalumu dhidi ya washtakiwa hao wa uhaini, isipokuwa mshtakiwa mmoja mwanamke mfanyabiashara na wenzake 21 ambao wamesomewa mashtaka matatu ya uhaini yanayowakabili.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Benson Bagonza amesema kuwa mashtaka hayo yatazidisha mvutano nchini.
Amesema, “Chaguo pekee la serikali sasa ni kudumisha amani na kuhuzunika na wananchi badala ya kuwakamata na kuwapeleka watu mahakamani.
Itakumbukwa kuwa wagombea wawili wakuu wa upinzani hawakushiriki kwenye kinyang'anyiro cha urais. Mmoja wao, ni kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha CHADEMA aliyeko kizuizini Tundu Antiphas Lissu, ambaye mwezi Aprili mwaka huu alishtakiwa kwa kosa la uhaini.