Rais wa Colombia amshambulia Trump: Wewe na marafiki zako ni waongo
-
Rais wa Colombia, Gustavo Petro
Rais wa Colombia, Gustavo Petro, amemshambulia Rais wa Marekani, Donald Trump, akionya kwamba kinachoendelea huko Gaza kinaweza pia kutokea Kusini mwa Dunia.
Gustavo Petro amesema kwamba "demokrasia imekufa duniani, na unyama ndio unaotawala," akikosoaji vikali sera za Magharibi na mfumo wa kibepari wa kimataifa, ambao ameutaja kuwa unaopendelea faida za kimaada kuliko uhai wa binadamu.
Katika hotuba yake ndefu, Petro ameeleza kwamba Colombia haijapokea silaha zozote za bure kutoka shirika la NATO, akisema: "Ni uongo kusema kwamba wametusaidia. Hakuna hata silaha moja ya bure iliyoletwa hapa nchini; tunanunua silaha za NATO."
Katika mashambulizi yake ya moja kwa moja dhidi ya Rais wa Marekani, Donald Trump, na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Marco Rubio, Rais wa Colombia amesema: "Ewe mrongo Trump na marafiki zako, wewe muongo Rubio, watu mnaowaua si wafanyabiashara wa dawa za kulevya. Wafanyabiashara wa dawa za kulevya ni wale walikwenda kwenye ofisini zenu huko Miami na kuomba mlipue mabomu mahali hapa, na mumuondoe madarakani rais aliyechaguliwa kwa kura ya wananchi, ili kujaribu kutudhalilisha."
Rais wa Colombia ameongeza kuwa mkutano wa hivi karibuni wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ulifichua kutengwa kwa Trump na Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, baada ya nchi nyingi za NATO kupiga kura ya kuiunga mkono Palestina chini ya shinikizo ya watu wao, akilitaja tukio hilo kuwa ni "wakati wa kihistoria ambao haujachambuliwa vya kutosha."
Gustavo Petro pia amekosoa "ushiriki wa serikali za nchi za Magharibi katika mauaji ya kimbari huko Gaza," akisema kwamba uhalifu dhidi ya "Flotilla ya Uhuru" katika Bahari ya Mediterania ulichochea hasira ya watu waliogundua kuwa serikali za nchi zao "zimeshiriki katika mauaji ya kimbari."