Nabih Berri: Haiwezekani kwa Lebanon kuanzisha uhusiano na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i132940-nabih_berri_haiwezekani_kwa_lebanon_kuanzisha_uhusiano_na_israel
Spika wa Bunge la Lebanon amesisitiza kuwa, yeyote anayetaka kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel anapaswa kujua kwamba, jambo kama hilo haliwezekani.
(last modified 2025-11-08T10:47:48+00:00 )
Nov 08, 2025 10:25 UTC
  • Nabih Berri: Haiwezekani kwa Lebanon kuanzisha uhusiano na utawala wa kizayuni wa Israel
    Nabih Berri: Haiwezekani kwa Lebanon kuanzisha uhusiano na utawala wa kizayuni wa Israel

Spika wa Bunge la Lebanon amesisitiza kuwa, yeyote anayetaka kuanzishwa uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Israel anapaswa kujua kwamba, jambo kama hilo haliwezekani.

Nabih Berri Spika wa Bunge la Lebanon, amesisitiza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kwamba kuanzisha uhusiano wa kawaida na adui Israel ni jambo lisilowezekana na kubainisha kwamba, "Vitisho na mashambulizi ya anga ya Israel dhidi ya Lebanon hayatabadili msimamo wetu."

Kwa mara nyingine tena Berri amesisitiza kufungamana na Lebanon na azimio la kamati ya "Mechanism" (inayosimamia utekelezaji wa usitishaji vita) na kusema kwamb,a inawezekana kutafuta msaada kutoka kwa wataalamu wa kiraia, kama ilivyofanywa kuhusiana na kuchora Blue Line mnamo 2000.

Kuhusu masuala ya ndani ya Lebanon, alisema bado hajapokea rasimu ya sheria ya uchaguzi iliyoidhinishwa na serikali na ataweka wazi msimamo wake kuhusu suala hilo baada ya kuipokea.

Akiashiria kwamba baadhi ya arakati za kisiasa kuhusu sheria ya uchaguzi ni ujanja usio na manufaa, Spika wa Bunge la Lebanon amesisitiza kuwa sheria hii ndiyo njia sahihi ya kutekeleza sheria.

Wakati huo huo, mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Lebanon, ambayo yamewaua shahidi na kuwajeruhi zaidi ya raia elfu moja wasio na hatia tangu yalipositishwa mapigano mwaka jana na kuharibu miundombinu na maeneo ya makazi, ni ukiukaji wa wazi wa uhuru wa kitaifa na umoja wa eneo lote la nchi huru na ni uhalifu mbaya dhidi ya amani na usalama wa kimataifa,".